Hii ni hatia au mlango wa neema?

Hii ni hatia au mlango wa neema?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,289
Reaction score
2,472
Mnakumbuka sakata la yule mama aliyesusiwa mapacha sita na mumewe. mwanamke aliachiwa watoto sita kwa madai kuwa anazaa sana.

Bila shaka alipitia kipindi kigumu sana hadi hapo alipofikia leo,leo hii mama huyu kwa neema za Mungu mama huyu anasomeshewa watoto wake kupitia wasamaria wema tena katika shule za maana.

Nachojiuliza ni kwamba, huyu baba aliyetelekeza familia ana kosa kiasi gani, hatuoni kwamba kupitia yeye huyu mwanamke na wanawe wameneemeka.

 
Kila mtu atalipwa kwa alichokitenda yeye.

Baba atalipwa kwa alichotenda na waliosaidia watalipwa kwa walichotenda.

Huwezi kuchukua wema wa wengine kama advantage kwa uovu wako.

Mambo yatahesabiwa separately.
 
Nachojiuliza ni kwamba, huyu baba aliyetelekeza familia ana kosa kiasi gani?

maandishi mekundu ni jibu la maandishi ya bluu...wajibu wa mzazi kwa familia ni kutunza na si kutelekeza

hatuoni kwamba kupitia yeye huyu mwanamke na wanawe wameneemeka?

...je unadhani ni sahihi kutenda dhambi kwa kuwa neema ipo?
 
Na hata hao watoto hawawezi kujakumuelewa huyo Mzee. Eti kama si mimi kuwatelekeza msingefika hapo.

Ni ujing.a wa hali ya juuvkabisa. Timiza wajibu wako mafanikio anatoa Mungu.
 
Huyo bwana kutelekeza familia ni big mistake and it's reward is punishment Mungu atajua adhabu yake ila haikua fair alichofanya.
 
maandishi mekundu ni jibu la maandishi ya bluu...wajibu wa mzazi kwa familia ni kutunza na si kutelekeza



...je unadhani ni sahihi kutenda dhambi kwa kuwa neema ipo?
Nilitafakari sana ndio maana nikaja kuwauliza na nyie. Hivi ile familia leo ingekuwa wapi kama bado wangekuwa na baba yao?
 
Unaweza fikiri una run from troubles kumbe una run from neema
 
Hiyo ni mbinu ya wanaume wengi kukwepa majukumu yao iwapo hali inabana.
Ila kisaidiwa sio neema bali kujidharirisha.
Kila nafsi inapaswa kujisimamia
 
Af baadae wakifanikiwa anarudisha sharubu nyumbani huku akijiita KICHWA CHA FAMILIA shwain...!!!
 
Back
Top Bottom