Hii ni CCM toleo la 4 na la mwisho; hakuna CCM nyingine baada ya hii!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Poleni UVCCM, Poleni sana!
Poleni LMB7, Poleni sana!
Poleni MATAGA, Poleni sana!
Poleni CHAWA wote, Poleni sana!

Hii ni CCM toleo la nne na kimsingi ndio toleo la mwisho, hakuna CCM nyingine baada ya hii!

Toleo la kwamza lilikuwa CCM asili ya Mwalimu Nyerere muasisi na rais wa kwanza wa Tanzania. Hapa hata CCM ya Mzee mwinyi rais wa pili wa Tanzania iko bado kwenye kundi hili la CCM toleo la kwanza

Toleo la pili lilikuwa CCM maslahi. Waasisi wa hili kundi ni marais Benjamin mkapa marehemu na Jakaya Kikwete mstaafu..hapa kigezo kikubwa ni mali, kipato na madaraka.

Hapa ndio vijana wa UVCCM maarufu kama LMB7 sana walipata umaarufu na nguvu kubwa..kwakuwa CCM maslahi waliwatumia vilivyo.

Toleo la tatu ni CCM makinikia. Muasisi wake akiwa ni marehemu John Pombe Magufuli..hawa walichujwa toka CCM asili na CCM maslahi, kisha akachanganya na wahamiaji wa kutosha sana!

Toleo la NNE ni CCM toleo la mwisho; ni CCM inayomezwa na wahamiaji wa kutosha na wasio na background na chama!

Simlaumu Mama Samia kwa hatua hii. CCM aliyorithi toka kwa mwanakwenda ilijaa chawa, wanafiki, watengeneza hujuma na kundi maarufu la MATAGA chini ya mwamvuli wa UVCCM/LMB7.

Hawa hawakuridhishwa na siasa za maridhiano za mama. Hawa hawakufurahishwa kabisa na hatua alizochukua mama kuwapeleka kizimbani makada maarufu wavunja sheria, haki za binadamu, waporaji na wala rushwa.

Hawa daily kwenye makundi yao, mitandaoni na kwenye vikao vyao hawakukoma kumkosoa bimkubwa na kumsema vibaya
Walichokisahau ni kimoja tuu kwamba wao wameshika makali na bimkubwa kashika mpini.

Teuzi mpya muhimu sana za wakuu wa wilaya zimesafisha karibia mabaki yote ya UVCCM, MATAGA NA LMB7. Ni kilio huko kwao. Ni msiba usio na matanga, wamenuna na kukunja sura. Hawaamini mama alichowafanyia!

Na hii ndio CCM toleo la mwisho. Baada ya hii hakuna CCM tena!

Ukipenda waeza hifadhi hii post kwa matumizi ya baadae!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Mama atapigwa uchaguzi asubuhi na mapema sana mwaka 2025 sio kwa chuki au kufanya vibaya Bali kwa falsafa ya mwanadamu ya ccm kuchokwa kama chama cha siasa chakavu zaidi Tanzania na Africa

Atashindwa uchaguzi asubuhi na mapema sana kwa jinsi anavyoenda ni kitu kimoja tu kinaenda kumuangusha nacho ni katiba mpya.

Ogopa sana zimwi na kuchakachua uchaguzi mwaka Jana hili zimwi ni hatari sana ndani ya watu uchaguzi ule uliacha makovu mengi na mama anajua Magufuli hakushinda na yeye yupo hapo kwa dhuruma ya utawala wa dicteta hakuna jambo kubwa kama Katiba na tume huru ya uchaguzi atalifanya na kufanikiwa kila akitaka kufanya maccm yatamwambia sisi ndio tumekuweka hapo tunataka ufanye ili na ili usifanye.

Atashutuka muda unaisha na hakuna atakachokifanya by 2025 hapo ndio upepo wa siasa za Tanzania utakapobadilika maana kutakuwa hakuna tena watu kutekwa kuchezea uchaguzi na watanzania watakuwa hawana cha kupoteza maana tatizo la Ajira mifumo ya elimu na mateso mengine ya kukatika kwa umeme na maji watakuwa na hasira navyo hivyo mambo yatakuwa magumu kwa mama na automatic kwa ccm.
 
Acheni kulazimisha upuuzi ambao kila mtu anaona ni upuuzi.
Kati ya wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa wahamamiaji wako wangapi Hadi useme UVCCM wanalia. Mbona karibia vijana wote walioteliwa ni wale wale, ha ha ha ha ha.

Hamsemi tu kuwa mnaumia kuona Nasaari ndani, Lijualikali ndani, Kalisti Lazaro ndani, Mtatiro ndani, Machali ndani, hata yule mwana wa Arusha ndani. Msilasimishe mambo.
 
Samia amekuja kuipaisha CCM kuliko Mwenyekiti yeyote tokea kiasisiwe, tunachosema aweke Tume HURU na wala asiogope; ili arudishe Legitimacy ya Utawala wake.

Wapinzani tutarudisha Majimbo yetu na kuongeza labda kiduchu, ila Mama ataongoza kwa Raha Mustarehe
 
Idugunde njooo!
JamiiForums-1847788434.jpg
 
Huyu Mama atapigwa uchaguzi asubuhi na mapema sana mwaka 2025 sio kwa chuki au kufanya vibaya Bali kwa falsafa ya mwanadamu ya ccm kuchokwa kama chama cha siasa chakavu zaidi Tanzania na Africa

Atashindwa uchaguzi asubuhi na mapema sana kwa jinsi anavyoenda ni kitu kimoja tu kinaenda kumuangusha nacho ni katiba mpya.

Ogopa sana zimwi na kuchakachua uchaguzi mwaka Jana hili zimwi ni hatari sana ndani ya watu uchaguzi ule uliacha makovu mengi na mama anajua Magufuli hakushinda na yeye yupo hapo kwa dhuruma ya utawala wa dicteta hakuna jambo kubwa kama Katiba na tume huru ya uchaguzi atalifanya na kufanikiwa kila akitaka kufanya maccm yatamwambia sisi ndio tumekuweka hapo tunataka ufanye ili na ili usifanye.

Atashutuka muda unaisha na hakuna atakachokifanya by 2025 hapo ndio upepo wa siasa za Tanzania utakapobadilika maana kutakuwa hakuna tena watu kutekwa kuchezea uchaguzi na watanzania watakuwa hawana cha kupoteza maana tatizo la Ajira mifumo ya elimu na mateso mengine ya kukatika kwa umeme na maji watakuwa na hasira navyo hivyo mambo yatakuwa magumu kwa mama na automatic kwa ccm.
CCM toka 2010 haijawahi kushinda kinachoshinda ni NEC
 
CCM inaenda kuongozwa na Kina Nassary, Mashinji, Lijuakali, Msando, Nick wapili, Jerry Muro na wahamiaji haramu kibao...
@BiaYetu
@Kawealumni
Crimea
Lizaboni
@Faixafoxy
Elitwege
Bashite
N.k wanaenda kuwa wapenzi watazamaji.
Kuna watu wanapambana sana kwa ajili yao lakini wao wanambulia vumbi tu,hii siyo haki
Mfano mtu kama Elitwege
Anapambana hadi anatoka na makamasi+povu

Ova
 
Back
Top Bottom