Hii ndoa inanivunja moyo, najuta kwanini nilimuoa huyu mwanamke

Habari wanajamvi, naombeni tumshauri huyu mwenzetu, kanisimulia mkasa wake mimi kama rafiki yake wa karibu sana
Huyu ndio tabia yake, anapenda sana kufuatilia simu yangu. Wakati mwingine anaiba simu yangu anachukua namba, anaanza kuwapigia watu anaoona calls zimeingia sana. Ana wivu wa kitoto sana
Jamaa we mwongo Sema ukweli bibie kakuta unaongea simu na mchepuko maana hata maandishi yako unaonekana ni uwongo.Unabahati umepata mwanamke hana hasira kakuchana na kisu kidogo laiti ningekuwa mimi ningehakikisha nakata kitendea kazi.
 

Ubongo wa mwanaume na mwanamke unavyofanya kazi ni vitu viwili tofauti kabisa..
Mwanamke hana subira hiyo mkuu inatakiwa uelewe utendaji kazi wa ubongo wao.

Wewe ndio mwanaume unasimama kama mkuu ndio mana ulipewa heshima ya kukojoa huku umesimama kwa ajili ya kuangalia usalama na kesho yake.
Sasa ukikimbia matatizo unazani nani atayatatua..??

Kwenye kikao mwanamke atasema nilimskia anasema nakuja kulala kwako leo
 
Alooh hali si hali!!
 
Mama nilikuwa nakutania
 
Ndoa nyingi sana sikuhizi ni Ndoano. Wanandoa wamepoteza nyuso za furaha muda wote wana mawazo sana, Wengine hudiriki kusema hadharani najuta kuoa/kuolewa na mtu huyu. Mungu awajaalieni busara za kuziishi ndoa zenu na Akili ya utatuzi wa changamoto mnazopitia.
 
Mkuu! mke anasameheka kwa kila jambo au kosa alifanyalo pasipo kujali chochote maana sisi wanaume huwachukulia kama watoto tu. Ila wasi wasi wangu ni hizo mbinu zake za kujihami siyo nzuri kabsa maana ipo siku kama utani atatoka na utumbo wako, Ogopa sana mtu anayetumia dhana za vita.. Hebu kubali kosa lako mbele ya wazazi wako plus wazazi wake then muulize why alifanya ivo? Uliza kama kwake ni sahihi kusimama mbele yako na hizo dhana? pia hoji kama wew ukizitumia ni sawaa kwake?, Then waachie wazazi wake wamkanye kwa hicho kitendo na uumpe mashariti yako katika nyumba yako mbele ya wazazi wote na mwelekeze haki yake anatakiwa aombe vipi endapo ataona anaonewa. Samehe rudi kuishi na mkeo mpya.
 
Mweleze Ukweli Kuhusu Simu Uliyokuwa unaongea nayo. Muweke Wazi na Umkanye Kwamba sio Kila ugomvi Wenu Lazima aupeleke Kwa ndugu. Mwambie haikukupendeza yeye kukushikia siraha. Jioni Ukirudi mletee kijizawadi Kisichozidi buku, Mwambie Unampenda na Unafanya hivyo Kwa maslahi ya ndoa yenu (huenda Mkeo anakupenda, ana wivu na wewe ila tu hakuamini maana hatujamskiliza na yeye). Mpe mwaka mwingine wa uangalizi.

Mwisho Kabsa,KUWA MWANAUME
 
Jamaa we mwongo Sema ukweli bibie kakuta unaongea simu na mchepuko maana hata maandishi yako unaonekana ni uwongo.Unabahati umepata mwanamke hana hasira kakuchana na kisu kidogo laiti ningekuwa mimi ningehakikisha nakata kitendea kazi.
angekuwa ni mchepuko kweli, nisingeona sababu ya kuficha. Nimuhofu nani huku nipo behind keyboard
 
Sina mpango wa kukaa kikao, ni kuwapotezea muda ndugu. Ila nitakuwa tayari kwenda ikiwa atalipeleka hili suala ktk neutral platform namaanisha kanisani
 
Mkuu wala sitaki ujitete hapo uliteleza kumpa confidence huyo mkewe ungeongea mbele yake halafu umpe maelezo kwa ufupi nani amekupigia simu sababu huyo ndo mwandani wako.....pole sana lakini
 
aah mkuu, mimi mwenyewe sikuamini kama angebeba hadi kisu, nikajisemea huyu kama kadiriki kuja na kisu live atashindwaje kuniwekea sumu kwenye chakula
Pole mkuu kumbe ni wewe nilidhani ni rafiki as you said.
 
Wakati ukiendelea kutafuta suluhisho hata baada ya suluhisho hakikisha hulali kizembe lala kimachale ulinde roho yako isinyofolewe na mai waifu wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…