TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
- Thread starter
- #41
Kilichofanyika ni kukarabati ile ya zamani jamani tusidanganyane
Abdallah, Mohamed Rished[CCM]
Pangani ConstituencySession NoQuestion NumberTo the Ministry of SectorDate Asked 1145INFRASTRUCTURE DEVELOPMENTCommunication/Infrastructure11 April 2008 Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa majibu ya matumaini aliyoyatoa jana, ambayo Wananchi wa Pangani wameyapata, lakini leo Mheshimiwa Waziri ametoa majibu ambayo matumaini yameanza kufifia.
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, suala la Kivuko cha Pangani, dharura ya sasa kwa muda wa mwaka mzima ni lazima tupate injini mpya kwa sababu tunahatarisha maisha ya wananchi mwaka mzima. Serikali wanasema hawataki kununua mashine mbili mpya; thamani ya roho za wananchi wale na injini mbili mpya ipi kubwa; mpaka tufe ndiyo tutaleta injini mbili mpya? Je, ni lini mtatununulia injini mbili mpya zifungwe katika Kivuko cha Pangani?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 45 SESSION # 11Answer From Hon.Mahanga, Dr. Milton Makongoro
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENTNAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU:
Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Rished Abdallah, kama ifuatavyo:-
Kwanza, nimpongeze kwa kweli kwa namna anavyofuatilia; ni kati ya Wabunge ambao ufuatiliaji wao katika matatizo ya wananchi wa majimbo yao ni mzuri sana.
Mheshimiwa Spika, lakini nimeeleza kwamba, kwa mujibu wa TANROADS mwezi huu wa nne kabla ya mwisho, tutakuwa tumetiliana saini kuleta kivuko kipya na kwa maana hiyo, itachukua mwaka mmoja kivuko kipya kuja.
Mheshimiwa Spika, lakini kama unavyojua, kwa uzoefu tulionao, injini ya vivuko kama hivi, pamoja na propeller yake ambayo inatakiwa vilevile, unapoagiza mchakato ule wote si chini ya miezi sita; huendi tu kuchukua na kesho ukawa umeleta injini kwa maana kwamba, tukileta na kwa matatizo ya fedha tuliyonayo ni kwamba, hata hiyo injini itafika karibu na kivuko chenyewe kipya kufika. Kwa hiyo, imeonekana ni busara kwamba, tuendelee kutengeneza hapa, yaani kukarabati injini na boti ile na sasa hivi tumepata maombi ya shilingi milioni 35, kwa ajili ya kukiweka katika hali nzuri, hela ambazo wizara yetu itadhamini kwa sababu TEMESA wana matatizo kidogo ili feri ile iendelee kufanya kazi kwa mwaka huu mmoja ambapo tunangojea feri mpya, kwa sababu kuleta injini nyingine itakuja wakati ambapo hiyo feri mpya nayo itakuwa inakaribia kufika.
Kazi kinafanya????