Hii ndiyo sababu ya matajiri kuwa na watoto wachache

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
UNAPO SHANGAA KWA NINI MATAJIRI WANA WATOTO WACHACHE, SHANGAA PIA KWANINI MASKINI WANA WATOTO WENGI.

Ila ukirudi katika hesabu utagundua kwanini mmoja maskini na mwingine tajiri.

Kwa malezi ya kistaarabu Mtoto mmoja gharama ya malezi yake hadi akifika chuo na kuanza kujitegemea ni miaka si chini ya 28 hadi 30.

Fanya kila siku katika malezi unatakiwa kuwekeza 5000 kwa mtoto kwa maisha yake yote toka tumboni, shule, mavazi, chakula na matibabu.

Tsh 5000 xsiku 30 x miezi 12 x miaka30=Jumla Tsh Milioni 54,000,000/- kwa mtoto mmoja katika malezi.

Ukimaliza malezi unakua amesha zeeka na kustafu..labda umebakisha miaka 10 au 15 mbele ya kuishi.

Sasa uamuzi ni wako chagua kuzaa watoto wacheche na hela ya watoto wengine uwekeze kwenye kununua hisa katika mabenki ujilee uzee wako wewe mwenyewe kwa kula hisa zako.

Au uzae watoto wengi uwekeze katika majukumu uitwe maskini na ubaki ukilaumu kuwa watoto hawakusaidii.

Wakatiohuo nao wapo katika majukumu yao ya msingi.
 
Vinginevyo Dunia ingeshuhudia wale wasiooa/kuolewa wangekuwa matajiri zaidi kuliko waliooa/kuolewa na hawana watoto. Na wale waliooa/kuolewa na wakawa na mtoto mmoja au wachache wangekuwa matajiri zaidi kuliko wenye watoto wengi. Binafsi nina watoto wengi na ninaishi vizuri kuliko baadhi ya watu wasiooa/kuolewa kabisa na hata wale wenye watoto kidogo pia. Utajiri umebebwa na mapambano yako wewe mwenyewe.
 
Idadi ya watoto haina mahusiano yeyote na kipato cha mtu. Ni maamuzi ya mtu binafsi.

Waarabu wana pesa mpaka hawajui cha kuzifanyia na unakuta mwamba mmoja ana wake 4 na kila mke ana watoto wasiopungua 5 na maisha ya kula bata yanaendelea kwa kila uzao.

Swala la idadi ya watoto lipo kitamaduni zaidi kuliko kiuchumi. Wazungu ni utamaduni wao kuwa na watoto wachache hakuna mahusiano na hali zao za kifedha.
 
Kwa hoja yako inaonyesha hesabu inakizi vigezo vya kujimudu, hii ikiwa na maana uwezo wako ni mkubwa unaweza kulea na kuendesha maisha yako bila kuteteleka mbeleni.

Maisha ni namba malezi ni namba watoto ni namba na namba moja ikizidi kuliko nyingine hasa namba hasi inaweza kuathiri mfumo

Kwa hivyo basi idadi sio mbili au tatu idadi sahihi ni ile ambayo HASI (-) haizidi CHANYA (+)...Through out....

Kama utaweza ku-maintain kopo la asali lisiishe dhidi ya walambaji na ukaweza kujitegemea mwishoni bado huja zidisha.

Hiyo kwa hapa INPUT must be greater than OUTPUT consistently
 
Idadi ya watoto haina mahusiano yeyote na kipato cha mtu. Ni maamuzi ya mtu binafsi.

Waarabu wana pesa mpaka hawajui cha kuzifanyia na unakuta mwamba mmoja ana wake 4 na kila mke ana watoto wasiopungua 5 na maisha ya kula bata yanaendelea kwa kila uzao.

Swala la idadi ya watoto lipo kitamaduni zaidi kuliko kiuchumi. Wazungu ni utamaduni wao kuwa na watoto wachache hakuna mahusiano na hali zao za kifedha.
Labda tusemeee Intput iwe kubwa kuliko output....

Na labda ujiulize uwezo wako na waarabu ni sawa...

Pia nimesemea watoto wengiiii ila sijataja idadi...take the NOTE..
 
Vinginevyo Dunia ingeshuhudia wale wasiooa/kuolewa wangekuwa matajiri zaidi kuliko waliooa/kuolewa na hawana watoto. Na wale waliooa/kuolewa na wakawa na mtoto mmoja au wachache wangekuwa matajiri zaidi kuliko wenye watoto wengi. Binafsi nina watoto wengi na ninaishi vizuri kuliko baadhi ya watu wasiooa/kuolewa kabisa na hata wale wenye watoto kidogo pia. Utajiri umebebwa na mapambano yako wewe mwenyewe.
Hivi watu haeayaoni haya?!Au ndo kukaa sana kwenye mageti!simple and clear ni mtizamo wako tuu na kupambana Maisha.
 
Back
Top Bottom