Hii ndiyo real change, ya Obama Slogan TU!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Wanafunzi wote walioomba mkopo wa kusoma Elimu ya juu wamepata, hii haijawahi kutokea tangu wimbi la vyuo na wanafunzi lilivyoikumba TanZania, na hii yote imewezekana ndani ya mwezi mmoja tu wa Magufuli wetu madarakani, hii sasa ndiyo ,,change we can believe in" ile ya Obama ilikuwa ni slogan tu!

Msisahahu pia sasa ni dhahabu yetu karibia itaanza kuchekechwa hapa hapa nyumbani badala ya mchanga kupelekwa nje ya nchi!
Pia kwa tajiri ameshindwa kununua Haki TanZania jambo ambalo siku chache zilizopita lilikuwa haliwezekani naam Manji amenyang'anywa Coco Beach na kurudishwa kwa wakazi wa Dar Es Salaam haya yote ndani ya mwezi mmoja tu madarakani, kunzia mwezi ujao hakuna ada wala mchango wowote ule kwa mtoto wa Kitanzania anayesoma kwa kifupi kusiwe na kisingizio cha mtoto kutokwenda shule haya yoote ndani ya mwezi mmoja Tu madarakani sasa kama hii siyo change we all can believe in basi labda sielewi maana ya hiyo sentensi!

Magufuli wetu hakunaga!

Barbarosa walioomba mikopo walikuwa wangapi na waliopewa ni wangapi, kiasi gani kilitengwa na kimetumika kiasi gani, hizo hela zilikuwa zimetengwa kwenye bajeti iliyopita au zimetolewa toka wapi, na huko zilikotolewa zimetolewa kwa kufuata utaratibu au ni ubabe wa kimadaraka umetumika?

Tatizo la mikopo limetatuliwa kabisa au hela zimetolewa kuonesha kwamba Magufuli "akiahidi anatekeleza?". Maana yangu jambo lenyewe limewekewa mkakati liwe la kudumu au ni mbwembwe tu za kuoneshana "Kasi" ili baadaye isemwe tena "Waliokopa hawajarudisha" kwa hivo serikali haina fedha?
 
Barbarosa walioomba mikopo walikuwa wangapi na waliopewa ni wangapi, kiasi gani kilitengwa na kimetumika kiasi gani, hiz hela zilikuwa zimetengwa kwenye bajeti iliyopita au zimetolewa toka wapi, na huko zilikotolewa zimetolewa kwa kufuata utaratibu au ni ubabe wa kimadaraka umetumika?

Tatizo la mikopo limetatuliwa kabisa au hela zimetolewa kuonesha kwamba Magufuli "akiahidi anatekeleza?". Maana yangu jambo lenyewe limewekewa mkakati liwe la kudumu au ni mbwembwe tu za kuoneshana "Kasi" ili baadaye isemwe tena "Waliokopa hawajarudisha" kwa hivo serikali haina hela?

Haijalishi cha muhimu Wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya kusoma wamepata, ambapo hapo awali walikosa fedha ilikotoka siyo muhimu hata kama tumekopa au tutalala njaa ili zipatikane fedha za na wanafunzi wasome yote heri TU, hapa muhimu klk yote ni kwamba tuna raisi ambaye anaelewa umuhimu wa Elimu na yuko tayari kufanya chochote kwa gharama yoyote ile ili wanafunzi wasome hapo nyuma tulikuwa tuko tayari kufanya chochote kwa gharama yoyote ile ili watu waende kwenye sijui kongamano gani Ulaya kukutana na Malkia wa Uingereza au kununua ndege ya raisi au sijui bilioni kwa kwa ajili ya vitafunwa na chai vya Ikulu na wageni wake!!
 
Barbarosa Kama kweli Magufuli anajali elimu inabidi awekeze kwenye kuelewa kuliko kwenye kusoma bila ya kuelewa. Wana CCM wenzako huko nyuma waliwahi kutuambia "hata kula nyasi tutakula" lakini ndege ya rais ni lazima inunuliwe. Hiyo tabia yenu ya kutokujali vyanzo vya mambo ndiyo mling'ang'ania kwamba hela iliyokuwa kwenye Tegeta Escrow siyo ya Umma wakati sasa tunaoshitakiwa ni Tannesco na Serikali ya Tanzania na siyo kina Tibaijuka.
 
Last edited by a moderator:

Magufuli wetu ana mwezi mmoja tu madarakani na mpaka sasa hivi amefanya yale yanayowezekana kulingana na hali halisi kwanza Wanafunzi waende shule hata kama wanakwenda kucheza nakurudi nyumbani jioni ni bora klk kukaa nyumbani na vijiweni kujifunza tabia mbaya kama wizi, kutumia madawa, umalaya n.k hivyo hapo baadaye hilo kuboresha Elimu ktk bora elimu kwenda kwenye elimu bora litafuatia taratibu lkn kwa sasa hivi waache waende shuleni!
 
Haijalishi cha muhimu Wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya kusoma wamepata, ambapo hapo awali walikosa fedha ilikotoka siyo muhimu hata kama tumekopa au tutalala njaa ili zipatikane fedha za na wanafunzi wasome yote heri TU, hapa muhimu klk yote ni kwamba tuna raisi ambaye anaelewa umuhimu wa Elimu na yuko tayari kufanya chochote kwa gharama yoyote ile ili wanafunzi wasome hapo nyuma tulikuwa tuko tayari kufanya chochote kwa gharama yoyote ile ili watu waende kwenye sijui kongamano gani Ulaya kukutana na Malkia wa Uingereza au kununua ndege ya raisi au sijui bilioni kwa kwa ajili ya vitafunwa na chai vya Ikulu na wageni wake!!
Huko nyuma no wapi? Ni kabla ya ccm kuwepo madarakani?au wakati ccm ikitawala? Na we we ulikuwa upande gani huko nyuma? Upande WA kusapoti?au WA kukemea? Na huko nyuma wanafiki walikuwepo pia? Au ndiyo wanaibuka enzi hii na kujifanya wanatetea kupinga mile walichokitetea kisipingwe? Jibu please
 
hebu muwe mnaangalia uhalisia mseongee takwimu mnazopewa....tupo tulioomba mkopo hatujapata mpaka leo halaf mnasema wote wamepata
 
Barbarosa Kama kweli Magufuli anajali elimu inabidi awekeze kwenye kuelewa kuliko kwenye kusoma bila ya kuelewa. Wana CCM wenzako huko nyuma waliwahi kutuambia "hata kula nyasi tutakula" lakini ndege ya rais ni lazima inunuliwe. Hiyo tabia yenu ya kutokujali vyanzo vya mambo ndiyo mling'ang'ania kwamba hela iliyokuwa kwenye Tegeta Escrow siyo ya Umma wakati sasa tunaoshitakiwa ni Tannesco na Serikali ya Tanzania na siyo kina Tibaijuka.
kweli atakua genius yaani awalazimishe watu waelewe...hata kama vichwa vyao ni 2MB
 
Back
Top Bottom