yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,635
- 3,658
HII NDIYO MAANA HALISI YA NENO KATERERO
Rafiki yangu mpendwa, naandika maneno haya nikiwa na uhakika kuwa yatakufikia na kuweza kukutoa katika kifungo cha mawazo. Ni wajibu wangu na ni haki yako pia, mimi kuweza kujitahidi kwa vyovyote vile niwevyo ili niweze kukutoa katika kifungo hicho.
Kuendelea kukuacha katika hicho kifungo eti kisa mimi sijafungwa kimwili, nitakuwa najidanganya kwani kama sijafungwa kimwili, nitafungwa kiroho. Ninaweza kukosa hata nafasi ya kuuonja utamu wa milele kwani nitakuwa na kesi ya kujibu huko mbeleni kwa maana Muweza Wa Yote anasema kuwa , “ Amuachaye mwenzie akaangamia ilihali anao uwezo wa kumnusuru atakuwa amejiangamiza yeye mwenyewe”.
Kwa mantiki hiyo sasa, nataka nikunusuru wewe usiangamie pamoja na mimi pia kwa kukutoa katika kifungo cha maana ya neno KATERERO.
Ikumbukwe kuwa ni wazi na ukweli usiopingika kuwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na upindishaji wa lazima wa maana ya neno KATERERO. Watu wengi tena wenye akili zao, ambao wangekuwa na uwezo wa kuwatoa wenzao katika dimbwi la maji machafu wameandika na wanazidi kuandika kiupotoshaji zaidi juu ya maana ya neno KATERERO.
Cha kusikitisha zaidi imefikia hatua sasa hata wale wenye nguvu kubwa sana kifedha na kiushawishi katika nchi yetu wamekuwa ni miongoni mwa wale wapotoshaji wa maana ya neno KATERERO.
Bora neno hilo lingekuwa na maana katika lugha nyingine za kibantu kusingekuwa na shida. Kinachofanyika ni kupotosha maana na kuihusianisha maana hiyo potofu na watu wanaotokea Kagera. Kwamba neno Katerero kwa Kihaya/ lugha nyingine za Kagera ina maaana….(maana potofu). Ni vizuri zaidi iwapo neno hilo kwa Kiha, Kikurya. Kimakonde. Kinyakyusa, Kipogoro n.k lingekuwa na maana hiyo inayolazimishwa.
Ukweli ni kwamba, ukijaribu kutarihi katika lugha zote za kibantu walau kwa hapa TANZANIA na kuangalia kama msamiati huu una maana nyingine huwezi kuikuta. Maana inayobakia na iliyotukuka ni ileile ya jina la Kata mojawapo katika Halmashauri ya Bukoba(v) .
Kata hizo za Halmashauri ya Bukoba (V). ni BUHENDANGABO, BUJUGO, BUTELANKUZI, BUCHULAGO, IBWERA, IZIMBYA, KAAGYA, KAIBANJA, KANYANGEREKO, KARABAGAINE, KASHARU, KATERERO, KATOMA, KATORO, KEMEONDO, KIBIRIZI, KIKOMERO, KISHANJE, KISHOGO, KYAMULAILE, MARUKU, MIKONI, MUGAJWALE, NYAKATO, NYAKIBIMBILI, RUBAFU, RUBALE, RUHUNGA pamoja na RUKOMA.
Neno Katerero kwa ndugu zetu wanyamahanga kwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, ndivyo linavyozidi kuonekana kama tusi kubwa sana mdomoni na akilini mwao. Hali hii inapelekea hata wale ndugu zetu ambao wanaishi kwenye huko kujiuliza mara mbilimbili kulitamka hilo neno hata kama kulikuwa kuna haja ya kufanya hivyo, hii ni kutokana na dhana potofu iliyojengeka kwenye akili za wanyamahanga walio wengi.
Kihistoria eneo ambalo hivisasa linaitwa KATERERO hapo zamani lilijulikana kama Kemondo. Ni eneo ambalo lilikuwa limechangamka sana, kwani kulikuwa na bishara nyingi sana zilizokuwa zinafanyika katika eneo hilo. Watu waliuza mazao, mahitaji, nguo na vitu mbalimbali katika eneo hilo.
Ni kutokana na kuchangamka kwa eneo hilo na upatikanaji wa pesa katika eneo hilo ndipo lilipopatikana jina KATERERO na hivyo kubadili jina la awali la Kemondo na kujulikana kama KATERERO. Ijapokuwa ubadilishaji huo wa jina haukuathiri eneo lote lililojulikana kama Kemondo, na ndio maana mpaka leo hii bado kuna sehemu inaitwa Kemondo.
Wenyeji na wafanyabiashara katika eneo hilo walikuwa wanapata pesa nyingi sana kutokana na wingi wa watu waliokuwa wanakuja kununua bidhaa. Ni kutokana na upatikanaji wa pesa huo, wenyeji hao walikuwa wanaambiana “Tugende KUTERA empiha/amaela-Twende tukakusanye/tukapige pesa).
Hifadhi akilini mwako kuwa, kitenzi KUTERA kwa Kiswahili kina maana ya KUPIGA. Ni kutokana na kitenzi hicho kuwa kimeambishwa tukawa tumepata neno KATERERO ambayo sasa kwa Kiswahili ikawa imebeba maana ya KUPIGIA. Kwa maana ya waliokusudia kuita jina hilo na pia kulingana na muktadha, walikuwa wanalenga dhana ya KUKUSANYA/KUPIGIA PESA.
Narudia tena kitenzi KATERERO (KUKUSANYA/KUPIGIA), kimetokana na kitenzi KUTERA (KUPIGA). KUPIGA/KUKUSANYA PESA ndiyo maana halisi na ambayo haina kigugumizi ndani yake kuhusu KATERERO.
Ndugu zangu WANYAMAHANGA ( watu ambao siyo wahaya), hiyo ndiyo maana halisi ya neno katerero ijapokuwa hamjakatazwa kukopa msamiati huo na kuutumia katika maana mtakayo nyie.
Mukama Kaiza (2017)
C & P