Hii ndiyo 'First eleven' ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo 'First eleven' ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMAPILI, AGOSTI 26, 2012 06:41 NA KULWA KAREDIA

  KARIBUNI tena wasomaji wangu katika safu yetu hii tuweze kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taifa letu. Moja ya jambo kubwa ambalo sasa liko mbele yetu ndugu zangu, ni Sensa ya Watu na Makazi ambayo imeanza rasmi usiku wa kuamkia leo.

  Hadi Sensa inaanza leo, imepitia milima na mabondeni kwa sababu wapo jamaa zangu fulani wanaosema hawataki kuhesabiwa! Jambo hili limenishangaza sana.

  Wameamua kulifanya jambo kuuubwa, hata kufikia hatua ya kusema hawako tayari kushirikisha waumini wao wahesabiwa! Jamani kweli taifa linaweza kuweka mipango ya maendeleo bila kuwa na idadi ya watu wake? Nadhani hii ni nadharia moja mbovu ambayo haipaswi kuungwa mkono na Mtanzania yeyote anayeipenda nchi yake.

  Tena, kibaya zaidi, hao ‘marafiki zangu' wanajenga hoja eti mazingira ya kutaka walipwe ‘viposho' ndiyo wawaruhusu waumini wao wahesabiwe. Nasema huu ni ‘ujinga' ambao haupaswi kuungwa mkono.

  Sasa msomaji wangu, baada ya Sensa kupita sijui watakuja na ajenda gani, maana yake wamekuwa mabingwa wa kuzalisha mambo halafu yanakufa kifo cha mende.

  Leo sitaki kujikita zaidi huko, lakini nimeona ni vema nikawakumbusha ‘marafiki zangu hawa' wakatambua umuhimu wa Sensa kwa maendeleo ya taifa.

  Leo mada yetu kuu inahusu Baraza la Mawaziri na utendaji kazi wao, ambao ama hakika nimeona ni bora tukauzungumzia kidogo. Unajua tangu Rais Jakaya Kikwete alipofanya mabadiliko miezi michache iliyopita tumeanza kuona matunda fulani.

  Wale ndugu waliokuwa wamezoea kututangazia mgao wa umeme, walipoachia ofisi, hivi sasa tunaishi maisha kama vile tuko Washington - Marekani ambako umeme kukatika huwa ni dhambi kwa taifa hilo.

  Baada ya wapiga kelele wengi na wafanyabishara hao, kuachia ofisi tumeanza kuona jinsi hatua kali zinavyochukuliwa na wale walioingia kuondoa ‘mibuyu' eti kwa lugha nyingine ambayo Watanzania wameizoea wanawaita vigogo.

  Siku hizi naona vigogo wameanza kuwaka matumbo joto, kama kuna mtu anabisha anipigie simu tushaurine.

  Hebu niambie msomaji wangu, pale kwenye chaka la TANESCO hakuna kigogo aliyepewa kadi nyekundu baada ya kuanzisha kampuni yake ndani ya shirika la umma, kisha akamteua mke na watoto kuwa viongozi? Jibu la hapa ni ndiyo tunamjua.

  Msomaji wangu, nani atabisha huko maliasili na utalii, vigogo waliosafirisha wanyama wapole kuliko wote duniani (twiga) nao wametupwa nje ya ulingo!

  Acha huko kule ambayo meli kubwa zinapiga nanga na kupakua ‘masunduku marefu' (makontena) nako kimewaka.

  Sasa naona nianze na ‘first eleven' ya Rais Kikwete ambayo naamini kama haitapata majeruhi inaweza kabisa kutuletea ushindi mzuri kwa taifa, baada ya kuwa kichwa cha mwendawazimu karibu miaka saba hii iliyopita.

  Mchezaji namba moja: Profesa Sospeter Muhongo (Wizara ya Nishati na Madini). Huyu tangu kuteuliwa kwake ameonekana kuwa lulu kubwa baada ya kuanika uozo uliokuwa ukifanywa na watangulizi wake.

  Angekuwa mchezaji wa mpira basi huyu tungemwita (Cristian Ronaldo kama siyo Lionel Messi) kutokana na mchango wake mkubwa kwenye kikosi chake.

  Amelihakikishia taifa hili kuwa halijawahi kupata mgao wa umeme tangu uhuru ila uliokuwapo ni wa kughushi tu! Jambo hili lilionekana kuwashutua watu wengi nikiwamo hata mimi.

  Profesa Muhongo pia ameweza kushusha gharama za kuunganishia wananchi umeme majumbani mwao. Watangulizi wake waliongoza kwa kututajia takwimu za uongo kila kukicha…. natambua wote mnawafahamu vizuri, sioni sababu ya kuwataja.

  Mchezaji namba mbili: Balozi Khamis Kagasheki (Waziri wa Maliasili na Utalii). Kwenye kikosi hiki anacheza nafasi ya kiungo (namba 6) kwa sababu amefanikiwa kugawa pasi ambazo zimezaa magoli (ana mapafu ya mbwa)

  Nasema hivyo kwa sababu tangu kuingia kwake hapo wizarani ameweza kuondoa ‘mibuyu' ambayo ilijiona yenyewe ndiyo yenyewe katika kutafuna rasimali za nchi hii na kuwasahau kabisa wananchi.

  Tangu kuingia kwake hapo, amefanikiwa kuwasimamisha kazi wakubwa ambao walishiriki kusafirisha wanyama wetu wakiwa hai, ingawa natambua wazi kwamba bado wengine wapo.

  Ameanza mikakati ya kupambana na mitandao inayoshirikiana na majangili katika mbuga zetu mbalimbali. Nasema huyu ni mchezaji mzuri kama hatapata majeraha ambayo yatamweka benchi. Unajua moja ya sifa ya mchezaji ni kucheza kikosi cha kwanza na kuisaidia timu.

  Mchezaji namba tatu. Dk. Harrison Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi). Huyu kama angekuwa mchezaji wa mpira yeye ndiye nahodha wa timu ambaye naweza kumfananisha na mchezaji nguli wa Italia, Paul Maldin. Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno kuongoza vema timu na kupanga mashambulio dhidi ya watendaji wazembe.

  Tangu akabidhiwe jukumu la kuongoza wizara hii, tumeshuhudia akichukua uamuzi mgumu, kama ule wa wiki hii wa kuwang'oa viongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na madai mbalimbali.

  Mtakumbuka moja ya malalamiko makubwa pale bandarini, yalikuwa wizi wa vifaa kwenye magari, wizi wa mafuta, ucheleweshaji mkubwa wa mizigo ya wateja jambo ambalo limesababisha nchi za jirani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Burundi, Rwanda na nyingine kuamua kuacha kutumia bandari hiyo na kuelekea Mombasa, Kenya.

  Huyu ndiye, amekuwa waziri wa kwanza kuamua kutumia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, nia yake ikiwa kujionea madudu ambayo yanawasibu Watanzania wa kipato cha chini.

  Mchezaji namba nne: Dk. John Pombe Magufuli (Waziri wa Ujenzi). Kama angekuwa mchezaji wa mpira huyo ni beki namba 5, kwani hacheki na mshambuliaji uwanjani.

  Anatambua namna ya kutimiza majukumu yake, anachukua uamuzi mgumu ambao kila Mtanzania anautambua. Ni muwazi na mkweli ambaye anajua namna ya kusimamia hoja zake za msingi.

  Katika timu huyu ni mchezaji ‘kiraka' kwa vile kila wizara aliyopelekwa ameonyesha ufanisi na utendaji mzuri.

  Katika ujenzi amefanikiwa kushusha gharama za ujenzi wa kilomita moja ya lami, amewafukuza makandarasi ‘walafi' kila kona, amevunja nyumba za watu waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara. Amewahi kumwambia Rais Kikwete amuache atimize majukumu yake.

  Mchezaji namba tano: Philipo Mulugo (Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi). Kama angekuwa mchezaji wa mpira huyu ni mlinzi wa kushoto. Anajua kupanda na kushuka kwa kupeleka mashambulio mbele kusaidia timu yake.

  Nasema hivyo kwa sababu tangu amekuwa naibu waziri, ameonekana wazi kumfunika waziri wake, Dk. Shukuru Kawambwa. Tumemshuhudia katika matukio mbalimbali ya taifa akipiga kelele nyingi zinazohusu wizara yake. Namuombea asipate majeraha wakati huu ambao mapambano yanaendelea kwa sababu akiumia anaweza akakuta nyavu za timu ya kijani zinatikisika.

  Mchezaji namba sita: Profesa Anna Tibaijuka (Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi). Kama angekuwa mchezaji anaweza kusema alianza kwa kasi kubwa, lakini alikujikuta hana pumzi ya kuhimili kucheza dakika 90.

  Inaonekana wazi kwamba hakuzingatia maelekezo ya kocha wake. Tulimshuhudia akithubutu kubomoa nyumba zilizojengwa ufukweni mwa bahari na kuta kadhaa katikati ya Jiji la Dar es Salaam, lakini ghafla amepotea uwanjani. Huyu sasa ni mchezaji majeruhi anayestahili kupata tiba ya kisasa arudi uwanjani.

  Mchezaji namba saba: Dk.Emanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani). Kama angekuwa mchezaji wa soka angecheza winga ya kulia, amekuwa mtu wa kupeleka mashambulio mazuri. Tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hii tumeshuhudia ile kasi ya polisi kusikia wanatesa watu na kuwapiga risasi imepungua kwa kiasi kikubwa. Nasema ajitihadi kuendelea na kiwango hicho taifa litafika linapohitaji.

  Mchezaji namba nane: Hawa Ghasia (Waziri wa TAMISEMI), kama angekuwa mchezaji wa mpira, ningeweza kusema kiwango chake kimeshuka mno, licha ya kusajiliwa kwa gharama kubwa. Nasema hivyo kwa sababu alitolewa Utumishi ambako alishindwa kumaliza tatizo la mishahara hewa ambayo imetafuna fedha nyingi za walipa kodi wa nchi hii.

  Lakini cha kusikitisha ni kwamba anatolewa Utumishi na kupelekwa TAMISEMI ambako huko ndiko kuna magenge ya walaji wasiokuwa na huruma na taifa hili.

  Yaani kama nilivyosema angekuwa mchezaji bado naweza kusema sijaona msaada wake hata kidogo kwa timu. Nasikitika kuona licha ya kiwango chake kushuka kocha bado anamng'ang'ania, sina hakika uhusiano wake na kocha ni wa namna gani!

  Mchezaji namba tisa: Samuel Sitta (Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki) kama angekuwa mchezaji wa mpira, basi yeye anacheza namba nne, kwa sababu ameweza kumudu safu nzima ya ulinzi. Tangu ameshika wizara hiyo hatujasikia manung'uniko makubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Amekuwa na msimamo wa kutetea nchi kwa kauli nzito. Kwa mfano suala la mpaka wa Malawi na Tanzania, tulimsikia namna alivyosimama kidete.

  Amekuwa mchapakazi muwazi kwa kila jambo liwe ndani ya chama chake au nje ya chama.

  Mchezaji namba 10: Profesa Jumanne Maghembe (Waziri wa Maji) kama angekuwa mchezaji, naweza kusema kiwango chake hakipandi wala hakishuki. Anastahili kucheza namba mbili.

  Tangu ameshika nafasi hiyo, amekuwa na mkakati mzito wa kuhakikisha makao makuu ya mikoa inapata maji kupunguza tatizo ambalo limekuwa likiwasumbua Watanzania. Namwambia kwamba Watanzania wanahitaji maji akaze msuli ni mchezaji mzuri.

  Mchezaji namba 11: William Mgimwa (Waziri wa Fedha) kama angekuwa mchezaji naweza kumfananisha na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba, Hussein Masha. Ni mchezaji mpole ambaye anapanga mashambulio bila papara. Tangu ameingia wizarani anapambana na mitandao ya wizi na kuhakikisha mianya yote inazibwa.Amekamata sehemu muhimu ambayo ni mhimili wa taifa, namshauri azidi kukaza buti.

  Namshauri kocha wa timu hii, wacheaji hawa wa akiba wapewe mazoezi ya ziada kurudisha viwango vyao, la sivyo wauzwe kabla ya pazia la usajili halijafungwa. Hawa ni Bernard Membe, Ummy Mwalimu, Gaudensia Kabaka, Dk. Makongoro Mahanga, Lazaro Nyalandu, Pereirra Silima, Gregori Teu, Samia Suluhu Hassan, Dk. David Mathayo David, Shamsi Vuai Nahodha, Adam Malima, Mathias Chikawe, Kapteni George Mkuchika, Profesa Makame Mbarawa, William Lukuvi na Dk. Mary Nagu.

  Kwa wale wachezaji waliopandishwa daraja hivi karibuni, Geroge Simbachawene, Dk. Charles Tizeba, January Makamba na Amos Makala, kwa ujumla viwango vimeanza kuridhisha.

  Wasomaji wangu, wiki ijayo tutaangalia wachezaji wa timu nyingine wanaocheza ligi ya mchangani (wabunge ambao hawako serikalini), kwani wapo mabingwa wa kupiga kelele kila mkutano wa Bunge unapoanza pale Dodoma.


  [​IMG]0713 207 553


  karedia2005@yahoo.co.uk
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Naona mwandishi kama anawapigia debe baadhi ya watu wasiofaa mfano Emanuel Nchimbi anayekabiliwa na tuhuma za kughushi. Amejitahidi kuandika ucheshi lakini ni mwanagezi asiyefikia viwango sawa na wenzake aliowaponda.
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  nilipoona hapo jina la Maghembe, Nchimbi na Hawa ghasia wala sikusoma tena hiyo habari maana ni meaningless kwangu!!
   
 4. d

  dada jane JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengine hujawataja mkuu kama dr Mahenge, Husein Mwinyi nk. Sio waakiba wala nini. So umewasahau au hawaeleki.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Mbona CCM wanamshutumu Director wa MTANZANIA - BASHE kuwa anaishutumu CCM? Sasa Mnashindwa kusoma habari?

  Ni vizuri kusoma kupata Uelekeo na kuweza kupinga au kusupport... Tukianza kuwa na Mawazo ya kupenda kusoma

  ​Tunavyovipenda kweli kutakuwa na DEMOKRASIA ya kweli NCHINI? AMKENI WAJAMENI...
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  Dr. MWINYI amefanya nini kwa Nchi? zaidi ya kukimbilia kwa Mzee Mwinyi? Ni Mkimya, Mmimi, Hana Marafiki kati ya Mawaziri

  Hana Marafiki kwenye Siasa za Nchi ila anatakiwa awe Rais wa NCHI...
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kwa Mulugo mmh
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  muda wangu huwa ni very precious nikishaona sentensi moja utumbo huwa siendelelei kusoma maana nasoma kitu ambacho dhamira yangu na akili yangu ilisha kireject that is my philosophy! i dont want to waste my time man!
   
 9. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  umeongelea vzr baadhi ya tuhuma za mafisadi wenu na sina tatizo na hlo...

  Tatzo langu na ww ni kwamba umeonesha kuridhishwa tu na hao mafisadi kufutwa ama kusimamishwa kazi zao.
  Mbn hawafilisiwi kma c unafki.... watu wanaibia nchi mabilion ya fedha af punishment kubwa mnayofanywa ni kuwafuta kaz tu... inasaidia nn..?

  Huyo Magembe kahamishwa wizara kibao lkn habebeki af bado unampa credibility......... duh we mkaree

  ww huna tofauti na wapambe wenzako.........
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Nchi gani hiyo anayoifukuzia maana so far nasikia watu wengine wanasema na yao ni nchi zaidi ya hii tunayoijua sisi.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hussein mwinyi ni mfanyabiashara zaidi kuliko mwanasiasa; nadhani siasa anafanya kwa kulazimishwa na baba yake kuwa pengine nae atakuja kuwa Rais!! He will be well advised to concentrate with his businesses because the chances of his ascendancy to the Union presidency are zero maybe the Zanzibar presidency in the absence of Dr.BILAL!!!!
   
 12. p

  pilau JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hiyo first eleven yako kuna wachezaji ambao wanaoumwa magoti na wengine ni wavivu wa mazoezi, wengine wanauza mechi na wapo wenye kusababisha penati katika kila mechi wanayocheza hevu weka benchi wengine acha Kagasheki, Muhongo, Mwakyembe, Magufuli,Tibaijuka, Mulugo, Sitta ongezea Mwanri
   
 13. L

  Lua JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hiki kikosi ni sawa na kikosi cha lipuli ya iringa, yenyewe inaongoza kwa kushuka daraja.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  LOL, Naona ndoto zake zitafifia sababu za UAMSHO na HAMAD kujitenga... Sidhani anaitaka ZANZIBAR pekee
   
 15. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  :biggrin1:
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Mbona urais umekuwa kazi nzuri...kila mtu ananusa na kunogewa
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hayo Ma-Account USWIS kila Mtu anataka kuwa nayo... URAIS BONGO MZURI... $$$ nje nje...
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Bila shaka mwandishi ametumwa huyo...
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Nchimbi kagushi nini? Mchawi mchukie lakini haki yake mpatie!
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kulwa Karedia, mdogo wake Jackton Manyerere! Nakuonea huruma kwa jinsi unavyojaribu ku-swim against the tide na kuhangaika kuwa mpgazi wa Bashe ambaye ni mtumishi wa wale ambao jamii ilishawapa hukumu na wanaishi kwa kujificha ficha. Haikushangaza kwa Gazeti la Mtanzania kuja na uharo huu, kwani hawana thamani zaidi ya hiki walichokiandika na haishangazi kwamba wakazi wa maeneo ya sinza madukani na kijiweni hujipatia makaratasi ya kufungia maandazi na vitumbua bure kutokana na kuporomoka kwa mauzo ya magazeti yao ya udaku.

  Fanya utavyofanya lakini kamwe uongo hauwezi kubatizwa kuwa ukweli na huyu Nchimbi, mwenye vyeti vya kununua, ambaye hajawahi hata kugusa matatizo ya wizara yake, achilia mbali huo upuuzi unaoupamba wa kupunguza vipigo vya polisi kwa raia, tunajua kwamba hata kuongoza nyumba yake hawezi. Kwa taarifa yako si tu kwamba polisi wanapiga, bali wanaua raia na ukibisha uliza tukio la Morogoro leo.

  Mtapatapa mpendavyo lakini malengo yenu kamwe hayatafanikiwa!
   
Loading...