Maambukizi mapya ya ukimwi, mimba zisizotarajiwa, zinaa holela, unyanyasaji wa kijinsia, kusimamisha shughuli za kiuchumi, uvutaji bhangi, ulevi, kutumia vibaya rasilimali na fedha za Taifa nk.
Kweli ni kichocheo cha maendeleo kwa wagonga meza na kupiga mayowe
Kwa maendeleo ya aina hiyo, na mimi naunga mkono kwamba kweli Mwenge ni kichocheo cha maendeleo. pia ni mahali pa kukuza unafiki. Tuseme tu kwamba kulikuwa na wakati Mwenge ulikuwa na maana kubwa tu, kama icon ya yale tunayoamini. Wakati huo Tanzania ikiwa nchi ya mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika. wakati huo Tanzania ikiwa ni sauti kali inayosikika duniani kote kupinga maonevu, unyonyaji, ukoloni, ukandamizaji. Hapo Mwenge ulilkuwa na maana. Wakati huo Siasa ni kilimo, katika kujenga taifa la wakulima na wafanyakazi. viwanda chekwa chekwa. ndani ya nchi Nyerere akihaha mikoani kusimamia kilimo, nje ya nchi kusimamia maslahi ya wanaoonewa popote duniani. Kuna wengi, wakiwemo waalimu maarufu katika Chuo Kikuu cha DSM na akina Mabala, waliovutiwa na misimamo ya Nyerere na wakaamua kuja Tanzania kupiga kazi.
Leo Tanzania hata haieleweki inasimamia kitu gani. Tumeanzisha mahusiano na mfalme wa Moroko, nchi inayokalia Sahara Magharibi kwa mabavu. Magu kamsujudia cheki bobu yule, akamomba amjengee msikiti na kitu gani sijui - uwanja wa mpira vile? Tumeanzisha mahusiano na Israeli, nchi inayomiliki taifa jingine la wapalestina, kama koloni lao. enzi hiyo hao wote walikuwa hawawezi kuisogelea Tanzania.
Enzi hizo TANU ilisema "BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRIKA NI MOJA" wakati huo usingesikia Nyerere anasema fulani siyo raia! Maana yake nini? wakati tunajenga Afrika moja, wakati mipaka iliwekwa na wakoloni ili watutawale? leo tunasema haya warundi nenda huko, wakati sisi wenyewe tukianza kuangaliana vizuri, ni Mgogo tu ndio mzaliwa wa nchi hii. lakini lengo siyo hilo. lengo ni kujenga Afrika iliyo imara na inayoamini katika usawa wa binadamu.
Ndani ya nchi hatueleweki pia. Kilimo tumekipiga kumbo, tunatangaza nchi ya viwanda wakati Nyerere hata hakusema hayo lakini alijenga viwanda vya kuheshimika. leo tunaongelea vyerehani vinne. Tunaporwa mali zetu kwa sababu ya upofu. Nyerere aliuona mchezo mzima akasema ngoja tujipange kwanza ndio tuchimbe madini yetu. Akaja Lofa Mkapa akatuingiza mkenge. Tuliingia kwa miswada ya dharura na kwa papara, leo tunataka kujinasua kwa miswada ya dharura na kwa papara vile vile. hatujifunzi tu?
Kifupi niseme tu kwamba Mwenge wakati ule kweli ulikuwa ni ishara ya mwanga wa Taifa la Tanzania kuangaza Afrika na dunia nzima. leo sisi ni kiiiza kinene. hatuwezi kuangaza popote. Mwenge umeshapoteza maana yake siku nyingi.