Hii ndio sababu ya watu kukimbilia siasa hasa nafasi ya Ubunge

Bee Network

Member
Nov 19, 2020
16
63
Takwimu zinaonesha kuwa mbunge analipwa mshahara wa shilingi milioni 3.8 kwa mwezi, posho ya mwezi shilingi milioni 8, posho ya kikao kimoja ni shilingi 240,000 kwa siku, posho ya kujikimu shilingi 120,000 kwa siku.

Baada ya miaka mitano ya ubunge wake anapokea pensheni ya shilingi milioni 240. Endapo mtu akichaguliwa kuwa mbunge anapata bima ya afya daraja la kwanza na familia yake, safari za nje ya nchi, pamoja na mishahara ya mbunge kutokuwa na makato ya mifuko ya jamii.

Tukiwaangalia Maprofesa nchini Tanzania wanalipwa mshahara takribani milioni 6 kwa mwezi lakini hawawezi kufikia pensheni hiyo asilani. Uprofesa wao watafanyia kazi miaka 30 hivi na hawatoweza kuambulia hata robo ya pensheni wanayopata wabunge. Wafanyakazi nchi hii hawapati maslahi makubwa kama wanayopata wabunge katika kipindi chao. Wafanyakazi na sekta nyingine hawana makazi ya kudumu, bima za afya za uhakika, mazingira ya kazi ni magumu.

"Kuliko idara nyingine yoyote, siasa imekuwa ni sehemu inayolipa zaidi".
 
Ndio maana sisi Chama Cha Mapinduzi tumeweka mchakato huru, wa haki na wazi katika kuchagua nani akatumikie wananchi kwa nafasi ya ubunge. Chini ya mwenyekiti wetu tumepata watu sahihi wakuwakilisha kero za jamii nchi nzima kwa serikali. Tofauti na hawa wanaojiita wapinzani huku wakisaka tonge tu !
 
Back
Top Bottom