Hii ndio sababu herufi za jina ambulance kuandikwa kutoka kulia kwenda kushoto

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,568
44,783
Labda sio mimi pekee niliyekuwa sifahamu, najua tuko wengi tuliokuwa hatufahamu ama tulikuwa tukifahamu bila ya kuwa na uhakika. Historia ya ambulance ilianzia Hispania na ujio wake katika ulimwengu wa kisasa ulianza miaka ya 1830s na hadi leo gari hili ni muhimu sana katika maisha yetu.

Gari hili huwa na king’ora, wakati mwingine msalaba mwekundu na taa inayowaka waka wakati likisafirisha mgonjwa mahututi. Na katika kila pembe huwa lina maandishi ‘Ambulance’ yaliyoandikwa kwa herufu kubwa kutoka kulia kwenda kushoto.

Madhumuni ya kuandikwa hivyo jina hilo ni kwa ajili ya kuwapa rahisi madereva wengine mbele ya ambulansi, kusoma vyema jina hilo kupitia kioo cha dereva.

Kawaida maandishi kwenye kioo huonekana tofauti na maandishi ya kawaida na ni kwa sababu hii ni bora kuandikwa kinyumenyume ili kusomeka vyema na rahisi katika kioo.

Screenshot_20190208-171559~2.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom