Hii ndio Passport ya Afrika iliyozinduliwa Rwanda

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450

Image captionBara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Je unamiliki cheti cha kusafiria cha taifa lako?

Hivi Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !

Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Madhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.


Image captionViongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Viongozi wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika.

Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.

Viongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.


Image captionMadhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.

Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.

Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.
 
Mimi sihitaji hiyo ya afrika nitaendelea kutumia passport yangu ya kimataifa, wao wangeondoa mambo ya passport na visa ingependeza sana

Kuna nchi zitafaidika sana na hii passport na kuna nchi zitaumia sana pia ,maana kuna nchi hazina fursa na watu wake wameshakata tamaa sasa kwa nchi nyingine kama zetu zitaumia sana kwa wahamiaji,
hapa nayaona matatizo wanayoyakimbia Ulaya yanahamia kwetu
 
Nmefurahi kuona maneno ya Kiswahili kwenye Passport
 
Inamaana walibya, wamisri,wasomali,wasudan kusini, wote waingie Tz? Mmh! Tutaumia
Na wewe pia unaruhusiwa kwenda kwao shida iko wapi?
Lakini seriously passport moja haimaanishi uhuru wa kuvuka mipaka.....mbona kuna passport ya EAC lakini jaribu kuvuka Namanga kiholela uone cha moto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…