Hii ndio operation red wing 28.05.2005

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,549
35,107
Mnamo siku ya tareh 27.06.2005 usiku…(makomando) wan ne vijana kutoka jeshi la marekani walishushwa katika kilele kimojawapo cha milima ya Hindu kush kijulikanacho kama (mountain tiger) na helkopita ya kisasa kabisa aina ya MH-47 Chinook.…na operesheni hii ilijulikana kama OPERATION RED WING au vita dhidi ya Abbas Ghar (kundi la talebani lililokuwa likiongozwa na Ahmad Shah) …mtu huyu alikuwa akiishi mashariki wa milima ya Hindu kush, Afghanstani karbia kabisa na mpaka wa Paksitani, ambaye alisadikika ni mmoja wa makamanda wa Osama Bin Ladeni

Ilikuwa tarehe 28.06.2005, ambayo kitengo cha kijeshi cha kimarekani maaruf kama US navy kitaikumbuka daima kwa kupotelewa na mashujaa wake 19 kwa siku moja…majeshi ya marekani yalikuwepo nchini afghanistani wakiendelea na harakati yake ya kumsaka Osama Bin Ladeni mtu ambaye aliaminika kuwa ndiye aliyeongoza mashambulizi ya September 11 mwaka 2001, lakini pia kuna jambo ambalo lilijitokeza na majeshi ya marekani yakaamua kulikabili, nalo lilikuwa kitendo cha magaidi kuamua kuvuruga harakati za uchaguzi uliokuwa ukitarajiwa nchini humo, na pia magaidi walikuwa wamepanga kuwaangamiza wote viongozi wapya watakaochaguliwa kwa kadri itakavyowezekana..

Tom wood afisa wa jeshi ambaye alihusika na eneo aliloishi gaidi Ahmad Shah alijadiliana na afisa mwenzake aliyejulikana kama Erik Kristensen ambaye alikuwa akisimamia kitengo maalum cha operesheni za kivita zilizohusisha wanajeshi maalum (makomando) na wakakubaliana kutuma kikosi maalum kwa ajili ya kumuua au kumteka Ahmad Shah..

Kwa kuanza walituma kikosi kwa ajili ya kupeleleza na kujua eneo sahihi alilpoishi Ahmad Shah..na hatua ya pili walituma kikosi cha pili kwa ajili ya kumteka au kumuua Ahmad Shah.. Tom Wood alipendekeza kuwa timu iende kwa mguu mpaka eneo husika badala ya kutumia chopa kuwapeleka na kuwashusha..kwani chopa lingeleta makelele na kuwastua watalebani…Erik kritensen alipinga ushauri huu na kupendekeza watumie chopa….wakatuma chopa ya kwanza ambayo ilishusha midoli mfano wa makomando katika maeneo mengi ili kuwapoteza maboya watalebani..badae zikafata chopa mbili na kwa haraka makomando wan ne walishushwa, zile chopa zilielekea huku na kule ili kuwavuruga wanamgambo wasijue kinachoendelea…hata hivyo mbinu waliyotumia ilihalalisha tu kushindwa kwao na kosa kubwa kabisa lilikuwa ni kuwashusha viwango magaidi....Na hata Marcus Luttrell komando pekee aliyesalimika anakiri wazi kuwa alihisi harufu ya kifo na kushindwa tangia mwanzo mwa operesheni..chopa liliwashusha katika kilele cha mlima, eneo ambalo lilikuwa tambarare(hakuna vichaka wala miti) kwa kiasi kikubwa hivyo kukosekana hata sehemu ya kujificha, eneo pia lilizungukwa na mapango pamoja na mabonde yenye mawe..na iliaminika kuwa chini ya mlima ndipo alipoishi Ahmad Shah…

Wakiwa juu ya mlima wenye urefu wa takriban futi 10000 kutoka usawa wa bahari…timu hii ilikabiliwa na changamoto kadhaa…Eneo lilikuwa tambarare, na walishuswa usiku wa mbalamwezi kiasi kwamba vivuli vyao vilikuwa vikionekana dhahiri, pia manyunyu ya mvua yalikuwepo, na ikumbukwe kuwa mazingira haya ndo makao ya talebani…uwepo wa majabali na maporomoko ulisababisha kukosekana kwa mawasiliano kati yao na wenzao.. mtambo wa redio aina ya (20 watt) PRC-117 ndo pekee ambao ungeweza kuhimili changamoto hii lakini hawakuweza kuwa nao sababu ya uzito na ukubwa wake…badala yake walikuwa na PRC- 148 MBITR ndogo Zaidi lakini yenye laini ya kuwezesha mawasiliano ya satellite...

Kwa nini makomando wanne

Kamanda Erick Kristenseni aliamua kutuma watu wanne tu kutokana na mazingira ya eneo, na pia kutokana na research waliokuwa wamefanya ilionyesha kuwa Ahmad Shah alikuwa na kikosi kidogo tu cha wanamgambo.…hivyo makomando wan ne walitumwa, wawili wenye utaalamu wa kutumia bunduki za shabaha (snipers) hawa walikuwa ni Marcus Luttrell(mlenga shabaha na daktari wa timu) na Matthew G. Axelson…wengine ni Michael P. Murphy (kiongozi wa msafara), na Danny Dietz (kiongozi wa mawasiliano).

Baada ya kushushwa walianza kutafta sehemu nzuri waweze kuwaona wanamgambo wa Talebani kwa urahisi Zaidi, na position nzuri Zaidi ya kuwakabili..asubuhi ya tareh 28 ilifika na ikapita, mnamo mda wa mchana, Luttrel alisikia vishindo vya mguu, kumbe walikuwa ni wachungaji wa Mbuzi wapatao watatu, watu wazima wawili na kijana mdogo mmoja, walikuwa hawana silaha Zaidi ya shoka za kukatia kuni, na walisisitiza kuwa wao sio talebani… waliwakamata na wakaanza kujadiliana wafanye nini..wawaue au wawaachie…walijua kabisa kuwa mara nyingi magaidi hutumia wachungaji kama chambo cha kujua walipo wanajeshi wa kimarekani, hata hivyo sio mara zote huwa hivyo..wengine huwa ni watu wema…hivyo kwa asilimia kubwa kuwaachia ilikuwa ni tiketi ya kifo kwao..na kuwaua watu ambao huna uhakika kama ni adui ni kosa kwa umoja wa mataifa kitengo cha haki za binadamu..

Walijaribu kuwasiliana na makao makuu namna ya kufanya lakini kulikuwa na bad network connection, chombo cha mawasiliano walichokuwa nacho hakikuwa na uwezo wa kuhimili geographical barrier ya eneo hilo ..hii ilimaanisha kuwa walikuwa eneo ambalo halipo accessible na mtandao, mwisho wakaamua kus sacrifice na kuwaacha waende zao..

Waliamua kuondoka hlo eneo , lakini kabla hawajafanya hivyo walisikia vishindo vya watu kutoka pande tatu…walijaribu kufanya mawasiliano lakini mtandao ulikuwa chini….waliamua kufa kiume, wakiwa wamewekwa mtu kati na wanamgambo wa talebani wapatao 30-50 hvi wenye AK45 na makombora aina ya (RPG)waliamua kupanbana huku dalili za kushindwa zikiwa dhahiri kutokana na mbinu za Ahmad Shah..

Murphy kiongozi wa timu..aliona sehemu sahihi ya kusalimika ni kushuka kwenye maporomoko kule chini akiamini kuwa wanaweza pata sehemu ya kujificha kwenye majabali na mapango.. hivyo waliamua kushuka chini bondeni…katika harakati za kupambana..Dietz alipigwa risasi mkononi na mgongoni..na kuvunja kidole, luttrell alivunjika nyonga sababu ya kujipigiza kwenye mawe na pia alikuwa amepigwa risasi moja kwenye paja, na akapoteza vifaa vya kitabibu hvyo iliwalazimu kupigana bila msaada wa kitabibu, Axelison alikuwa amepigwa risasi mbili mgongoni na kifuani…

Sheria za jeshi la marekani ni kosa la jinai kumwacha majeruhi mwenzako kwenye uwanja wa vita..ni heri kufa nae, hivyo Lutrell aliamua jukumu la kumburuza Dietz huku dietz akiendelea kufyatua risasi ili kupunguza nguvu ya maadui dhidi yao na kuwaokoa wenzake, Dietz alipigwa risasi mbili moja kifuani na nyingine kichwani, Dietz kijana wa miaka 25 alikufa mikononi mwa Lutrell…

Mpaka mda huu walibaki askari watatu wa Navy waliokuwa serious injured..walifika sehemu ambayo ndo pekee salama kwao (mapango)..kwani mbele yao hakukuwa na sehemu nyingine ya kujificha..akiwa chini ya jabali..Murphy alijaribu kufanya mawasiliano ya satellite lakni kukawa na bad network..Murphy aliamua kupanda juu ya jiwe katika harakati za kutafta msaada, huu ulikuwa uamzi wa kujitoa mhanga kwani juu ya jiwe angeonekana dhahiri mbele ya maadui, alipigwa risasi kifuani lakini akafanikiwa kufanya mawasiliano na headquarters na kuwaambia “vijana wangu wanakufa hapa, tunahtaji msaada” alipigwa risasi nyingine mgongoni, alifanikiwa kuchukua silaha yake na kufyatua risasi kadhaa, aliita “Lutrell nisaidie” kabla ya sauti yake kutulia kimya kabisa…

Kama matokeo ya mawasiliano aliyofanya Muphy, Chopa aina ya MH-47 chinook ilifika eneo la vita , kamanda Erick Kristenseni na wengine 15 walikuwemo ndani ya chopa…wakijua kabisa kuapproach hot batlle area is very dangerous , waliamua tu kushuka katikati ya uwanja wa vita kuku wakipiga risasi ili kunetralize wanamgambo, jambo hili walilifanya kutokana na hali ya wenzao waliokuwa wakihtaji msaada wa haraka Zaidi…bila kuchelewa taleban waliachia kombora (RPG) lililotungua ile chopa…askari wote 16 pamoja na kamanda Erick Kristenseni waliangamia

Lutrell alishikilia mkono wa Axelson, Axelson alimwambia kuwa "naamini Luttrell utaokoka, na endapo itakuwa hivyo kamwambie mke wangu Cindy nampenda sana" lakini kabla hajamalizia kauli, wote wawili walipigwa kombora (RPG) toka kwa talebani lililowatenganisha wote wawili, Lutrell hakumuona Axelson tena…Axelson alikuwa na bastola na magazine tatu, mwili wake ulipopatikana siku saba badae magazine moja tu ndo ilikuwa imebaki bila kutumika....hivyo kuna uwezekano mkubwa aliendelea kupambana kabla hajafa...
Luttrell alifanikiwa kuondoka kwenye uwanja wa vita akijivuta umbali wa km 11 hvi pembeni ya mlima hadi alipookotwa na wasamalia wema….waliomtunza hadi july 2 walipotoa taarifa kwa kambi ya kimarekani iliyokuwa karibu…ambayo ilituma kikosi na kumuokoa..mda wote huu taleban wakiuwa wakija mara kwa mara pale kijijini wakitaka wamsalimishe Lutrell, hata hivyo hawakufanikiwa…na baada ya kuokolewa kwa Lutrell familia iliyomuokota ilihamishiwa Califonia Marekani kutokana na vitisho vya talebani…Tangu vita ya pili ya dunia marekani ilikuwa haijapoteza wanajeshi wengi kiasi hcho ndani ya siku moja katika uwanja wa vita…Na kitengo cha operesheni maalum cha Nav kilikuwa hakijawah kupoteza askari wengi tangu kuanzishwa kwake… Murphy alitunukiwa tuzo ya juu ya heshima kwa kitendo chake cha kujitoa mhanga ili kuokoa wenzake…Dietz, Lutrell, na axelson walitunukiwa tuzo kwa ushujaa wao…na kila tareh 28.05 kila mwaka jeshi la marekani hufanya maazimisho ya kumbukumbu…(Operation wing memorial day)

Lutrell ndo mhanga pekee aliyeokoka..na alifanyiwa operesheni 15 kutokana na majeraha mbalimbali aliyopata….mwaka 2010 alistaafu masuala ya kijeshi na akafunga ndoa kwa sasa ana watoto wawili….Mwaka 2007 aliandika kitabu cha Lone survivor ambacho kilitumika kutengeneza filamu ya “LONE SURVIVOR” mwaka 2013..katika filamu kuna matukio yameongezwa ambayo hayakutokea, mfano mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la marekani ili kumuokoa Luttrell hayakuwa real, Luttrell alihifadhiwa tu na familia ya Gulab kwa mda wa siku tatu hadi badae alipoochukuliwa..taleban waliwaua baadhi ya wanafamilia wa gulab na kuchoma gari lake, kama harakati ya kushinikiza wamtoe Luttrell, ila jamaa alikaza kutomtoa..., kwenye filamu pia inaonesha kuwa Dietz alizungukwa na wanamgambo kabla ya kufa, Lakini kiuhalisia Dietz alikuwa ameshakufa tena mikononi mwa Luttrell..

Hapo chini ni picha ya Kamanda Michael Murphy Enzi za uhai wake

murph_radfordm.jpg

Hapo chini ni Marcus Luttrell na mkewe, Luttrell ni askari pekee aliyesalimika katika operation red wing 28.05.2005

7757bed33e85f145983821e3ec88bbf7.jpeg

Picha hapo chini ni Mathew Axelson akiwa na mkewe (cindy) enzi za uhai wake,
1a71c4204fd44b2b46b9591ca6db1443.jpg
cindy-and-matthew-axelson-6-pic.jpg

Hapo chini Kijana Danny Dietz enzi za uhai wake akiwa na mkewe
love.jpg

Chopa aina ya MH-47 Chinook
873.jpg

Mohamed Gulab ndiye aliyemuokoa Marcus Luttrell
0520gulab05.jpg

Waigizaji katika filamu ya Lone survivor
image.jpg

Karbuni wadau
 
Boonge la story Umenipa mwanga hiyo movie 'Lone Survival'Nilikuwa nayo kiukweli sikuipenda maana sikuelewa mpaka Nikaifuta but leo Nimejua kisa chake.
 
Bila shaka hiyo movie ina mambo ya kujifunza.

Shukrani kwa thread nzuri.
 
Kinachonishangaza ni kuwa nikiangalia lone survivor movie kuna sehemu Marcus luttrrel original anaonekana,, wakati wako wanapewa maekekezo kuna jamaa kaweka miwani kichwani kafanana sana na murcus
 
  • Thanks
Reactions: SDG

inatisha sana
 
Asaante kwa makala hii. Niliiangalia movie waliyoigiza hii stori. Du ni hatari
 
Back
Top Bottom