Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,199
- 7,562
"Kujijengea tabia ya kufanya vitu kwa namna na katika viwango ambavyo ungependa kila mtu afanye vivyo hivyo,kumfanyia mwingine ambacho ungependa nawe ufanyiwe na kufanya vitu katika kiwango ambacho ungetamani iwe standadi ya ulimwegu ndio msingi mkuu wa Uadilifu na ubinadamu" (E. Kant).
Basi awezaye kuufuta msingi huu uliojaa hekima na aufuate kwa ustawi wa jamii ya mwanadamu.
Wala usijaribu kunitisha eti nitapoteza mvuto wa kisiasa halafu ntakosa kura.Ebo! mimi si wanasiasa na wala sitafuti kura.Ni mwalimu ninayekufundishia watoto wako.
Basi awezaye kuufuta msingi huu uliojaa hekima na aufuate kwa ustawi wa jamii ya mwanadamu.
Wala usijaribu kunitisha eti nitapoteza mvuto wa kisiasa halafu ntakosa kura.Ebo! mimi si wanasiasa na wala sitafuti kura.Ni mwalimu ninayekufundishia watoto wako.
Ubakaji ni uhuni na kitendo cha kinyama kisichokubalika, yeyote anayebaka anatakiwa kupigwa vita bila ya kujali ni nani!,
Wizi ni uovu, unapaswa kukemewa bila kujali nani anaiba!,
Uongo na ulaghai ni uovu, unatakiwa ukemewe bila kujali nani anaufanya. Huo ndio msingi wa uungwana na hekima kwa jamii ya watu wastaarabu wanaojitambua.
Kitendo cha kukemea uovu unapofanywa na mtu fulani, lakini uovu huo huo ukifanywa na mtu mwingine unachekelea na kushangilia, ni kinyume na misingi ya ustaarabu na utu.Haiyumkiniki unalalama mwanao anapodhulumiwa na kujifanya wewe ni mtu wa haki sana, ila anapodhulumu unashangilia , na kwa bahati mbaya watanzania wengi tumejikuta katika kundi hili.
Haiyumkiniki tukawa tunadai sisi ni waumini wa demokrasia, tukadai vyama vingi ili kupanua demokrasia, tukadai chaguzi huru na haki za mara kwa mara ili kupanua demokrasia n.k halafu watu hao hao tukawa tunashabikia watu wanaozuia demokrasia ndani ya vyama vinavyodai kuanzishwa ili kutetea na kukuza demokrasia.
Haiyumkiniki; Sisi sisi ndio tunaolalamika kwamba chama tawala (kinachofanya chaguzi kwa ngazi zote mara kwa mara kwa mujibu wa katiba yao) kuwa wanawekana kwa misingi ya kindugu, hawana demokrasia n.k, kisha na sisi tunaanzisha vyama kwa kukipinga halafu tunafanya vivyo hivyo au zaidi ya hivyo halafu tunateteana na kupongezana kisa tumkomoe fulani.
Sisi ndio tunaodai twataka demokrasia, lakini kuna vyama mwanyekiti ni mume katibu mke, halafu mara tunakemea, tukiona maslahi upende wetu mara tunatetea, mara leo tunalalamika mara kesho tunawatetea kwa kukumbatia tabia hiyo hiyo.
Haiyumkiniki; sisi tunaodai demokrasia na kuanzisha vyama kwa hoja ya kupanua demokrasia, halafu ndani yetu kuna watu wanapambana na hiyo demokrasia yenyewe kwa ndani (kwa kutotaka uchaguzi huru na haki), halafu kwa nje wanadai kuipigania hiyo demokrasia na sisi tunawapigia vigelegele.
Haiyumkiniki mtu ukiyasema haya unaambiwa kwa nini huwaambii wale, kana kwamba kuna wenyehaki ya kufanya uovu kuliko ilivyo kwa wengine.
Nasema hivi: Kambi yangu ni ya wapenda demokrasia daima.Kokote nitakapoiona demokrasia nitaitetea.Yeyote atakayeitetea na kuisimamia nitamuunga mkono na yeyete atakayeisigina nitamkosoa.Demokrasia ni pamoja na chaguzi huru na haki na za mara kwa mara.Yeyote anayependa na kutea kufanyika chaguzi za mara kwa mara, huru na haki katika level na nyanja zote nitamuunga mkono. Hiyo ndio kambi yangu na anayetaka kujiunga na kambi hiyo naajiunge na asiyetaka aache!.
Watu wanaulizana, wewe uko kambi ya nani au nani? waambie niko kambi ya wapenda uadilifu kwa dhati ya moyo wangu. kambi ya wapenda uchaguzi huru na haki, niko kambi ya wanaotenda yale wanayopenda kutendewa na nitabaki hivyo daima.
Kama unafikiri ni busara kuchagua kambi hii inayosimamia misingi karibu, kinyume chake chagua kambi utakayo wewe maana binadamu hawafanani wngine wanafanya kazi, wengine omba omba, wengine wezi, wengine panya road lakini maisha yanaenda.Dunia ndivyo ilivyo!