Hii ndio hali halisi Syria, inasikitisha sana

Picha ya mvulana wa Syria iliyowasikitisha weng

_90842401_aleppo_boy_amc.jpg

Image captionMvulana Omran mwenye umri wa miaka minne
Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la kubebea wagonjwa Syria, imeweka wazi tena madhila wanayopitia raia nchini Syria.

Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.

Picha hiyo ya Omran, 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana katika ufukwe wa Uturuki mwaka jana.

Omran alitolewa kwenye vifusi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la kutoka angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.

Jamii ya kimataifa imeguswa na wito wa kusitishwa kwa mapigano kutolewa.

Mshirika mkuu wa Rais Bashar al-Assad, Urusi, imesema iko tayari kusitisha vita katika mji huo wa kaskazini kwa saa 48 kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.

"Nimepiga picha nyingi za watoto waliouawa au kujeruhiwa wakati wa mashambulio yanayotekelezwa kila siku," mpiga picha hiyo Mahmoud Rslan aliambia AFP.

"Kawaida, huwa wamepoteza fahamu au wanalia. Lakini Omran alikuwa amekaa hapo, bila kutamka neno, akionekana kuduwaa, kana kwamba hakuwa anafahamu nini kilichokuwa kimetokea."

_90842515_0b54839e-af8d-4937-a7d2-b5838e409b8e.jpg

Image caption Mwili wa Ayran Kurdi ukiondolewa kwenye ufukwe wa bahari Uturuki mwaka jana. Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini Syria.

Zaidi ya watu 17,700 wanakadiriwa kufariki wakiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.

Sasa hapo anapanda ndege akiwa hivyo mchafu, alikuwa anapelekwa ukimbizini au? Basi hapo utawaona wale ndugu zetu waliokimbilia Somalia miaka ya nyuma kuomba wapelekwe Syria wakahifadhiwe huko wakati wazawa wenyewe wanapakimbia.
 
Juzi juzi wameanza tena kutumia gas ya sumu kule aleppo....Mashirika ya misaada ya UN wamegundua kwamba majeshi ya Assad wametumia gas ya sumu aina ya 'White Phosphorus'..Ata sijua haya mashambulizi ya anga faida yake nini,Sijawahi kuona civil war ikiamuliwa kwa Air strike zaidi ya kuuwa wasio na hatia na kuleta uhasama baina ya watu na serikali yao...Poor syria,imegeuka uwanga wa kujaribu sulaha mpya za Urusi.
 
Mm najiuliza sana yote haya ni kwasababu ya mali?
 
Pia kwanini inch kama Turkey, Jodarn, Iran, Saudi arabia, Pakistan na Egypt zote hazitoe msaada kwa wakimbilizi hata kuwapokea. Naona inch kama Germany ndio inajitaidi kutoa msaada
 
Picha ya mvulana wa Syria iliyowasikitisha weng

_90842401_aleppo_boy_amc.jpg

Image captionMvulana Omran mwenye umri wa miaka minne
Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la kubebea wagonjwa Syria, imeweka wazi tena madhila wanayopitia raia nchini Syria.

Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.

Picha hiyo ya Omran, 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana katika ufukwe wa Uturuki mwaka jana.

Omran alitolewa kwenye vifusi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la kutoka angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.

Jamii ya kimataifa imeguswa na wito wa kusitishwa kwa mapigano kutolewa.

Mshirika mkuu wa Rais Bashar al-Assad, Urusi, imesema iko tayari kusitisha vita katika mji huo wa kaskazini kwa saa 48 kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.

"Nimepiga picha nyingi za watoto waliouawa au kujeruhiwa wakati wa mashambulio yanayotekelezwa kila siku," mpiga picha hiyo Mahmoud Rslan aliambia AFP.

"Kawaida, huwa wamepoteza fahamu au wanalia. Lakini Omran alikuwa amekaa hapo, bila kutamka neno, akionekana kuduwaa, kana kwamba hakuwa anafahamu nini kilichokuwa kimetokea."

_90842515_0b54839e-af8d-4937-a7d2-b5838e409b8e.jpg

Image caption Mwili wa Ayran Kurdi ukiondolewa kwenye ufukwe wa bahari Uturuki mwaka jana. Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini Syria.

Zaidi ya watu 17,700 wanakadiriwa kufariki wakiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.
Unaisikitikia Syria wakat,Kongo DRC watu wanakufa,Sudani kusini watoto wanakufa na njaa,chibok girls hadi leo hawajarudi kwa wazazi wao??
Habari za Syria zipo nje ya uwezo wetu.Tuisikitikie Afrika kwanza ndipo twende huko Syria.
Tatizo vijana mnakopi sana habari za kwenye mitandao ambazo zinaandikwa kwa masrahi ya watu wengine kwa sababu zao wenyewe.
Ni kweli Syria hali mbaya lakini sudani kusini hali mbaya zaidi.
 
Hapo ndo utaona HIPOCRISY
Picha ya mvulana wa Syria iliyowasikitisha weng

_90842401_aleppo_boy_amc.jpg

Hapa ndo utaona HIPOCRISY ya hawa waungwana wa saudia na iran.ingekua mtoto huyu ni wa KIPALESTINA aiyenusurika shambulio la ndege vita ya MAYAHUDI,ungewaona leo baada ya swala la ijumaa pale msikiti maarufu wa kko wamemwagika mitaani WAKIANDAMANA kulaani na kuonyesha SOLIDARITY na hao WAFILISTI,
SASA NASHINDWA KUELEWA MAISHA YA HAWA WAFILISTI NA WAASYRIA YANA THAMANI TOFAUTI
 
Wanasababisha..wanapiganisha.wanasuluhisha.wWanaweka vibaraka Wao. Hii ndo dunia
 
Sasa hapo anapanda ndege akiwa hivyo mchafu, alikuwa anapelekwa ukimbizini au? Basi hapo utawaona wale ndugu zetu waliokimbilia Somalia miaka ya nyuma kuomba wapelekwe Syria wakahifadhiwe huko wakati wazawa wenyewe wanapakimbia.

Nani kakuambia hiyo ni ndege? Hiyo ni gari ya kubebea wagonjwa
 
Unaisikitikia Syria wakat,Kongo DRC watu wanakufa,Sudani kusini watoto wanakufa na njaa,chibok girls hadi leo hawajarudi kwa wazazi wao??
Habari za Syria zipo nje ya uwezo wetu.Tuisikitikie Afrika kwanza ndipo twende huko Syria.
Tatizo vijana mnakopi sana habari za kwenye mitandao ambazo zinaandikwa kwa masrahi ya watu wengine kwa sababu zao wenyewe.
Ni kweli Syria hali mbaya lakini sudani kusini hali mbaya zaidi.

Mleta uzi yupo sahihi, wewe ndiye upo wrong! Hakuna ulichoongea cha maana yote pumba tupu! umeonyesha ubaguzi wa hali ya juu mno,na nadiriki kusema "wewe ni mbaguzi" ndio maana taarifa hii haijakugusa, na lau km imekugusa usingethubutu kuongea upuuzi huo, kama vipi anzisha mada yako hujazuiwa, Ungejua humu kuna taarifa nyingi tu za africa na tunazifatilia 24hrs labda kama sio mfatiliaji wa habari,

Duh waafrika tuna safari ndefu kweli kweli, embu tujirekebishe bwana.
 
Asaad achia nchi hiyo wape wengine,ni Mungu pekee ndio mwenye utawala usio na kikomo, tuliobakia lazima tutawale kwa zamu ndio mambo yaende sawa.
 
Hii ni Vita ya mataifa makubwa. Huku marekani huku Russia. Wanaoteseka si Assad ni waraia masikini wasio na uwezo wa kijitetea. InshaAllah mwenyeeziMungu atawaokoa na madhila wanayopitia.
 
Mleta uzi yupo sahihi, wewe ndiye upo wrong! Hakuna ulichoongea cha maana yote pumba tupu! umeonyesha ubaguzi wa hali ya juu mno,na nadiriki kusema "wewe ni mbaguzi" ndio maana taarifa hii haijakugusa, na lau km imekugusa usingethubutu kuongea upuuzi huo, kama vipi anzisha mada yako hujazuiwa, Ungejua humu kuna taarifa nyingi tu za africa na tunazifatilia 24hrs labda kama sio mfatiliaji wa habari,

Duh waafrika tuna safari ndefu kweli kweli, embu tujirekebishe bwana.
Umetoka povu jingi mdomoni,ubaguzi wangu ni upi sasa? Bado tuna majanga makubwa hapa Afrika kuliko huyo Mtoto ambaye amechubuka tu usoni amejaa na vumbi usoni lakini ni mzima tu wa afya; huwez kufananisha na makumi ya watoto wa chiboko ambao wanabakwa na kuuawa na boko haram,videos za mateso yao tunaziona.Tatizo hizo habar za Syria zinatangazwa sana kutokana na pande mbili zinazokinzana na kila pande inatafutwa kuungwa mkono kimataifa.
Hivi juzi tu hapa pale Kongo kwa Joseph kabila watu karibu 200 wameuawa kwa mapanga lakini hatusikii wa Afrika au vyombo vya habari vya kimataifa vikiangazia sana habari hizo lakini tunaandika habar za uarabuni huko za mtoto kakoswa na Bomu ndoinakuwa habar kuuuuubwaaa.
Tatizo sisi wa Afrika tunashindwa kutangaza habari zetu kwa nguvu na baadae tunapenda sana kutangaza habar ambazo zipo nje ya uwezo wetu au hazituhusu kabisa.Utaona gaidi labda kawaua watu ufaransa huko eti wewe mgogo wa Tanzania nawe unabadili profile picha ya Facebook yako kuonesha mshikamoni na watu wa Paris, ufaransa,wakat mauaji ya West gate Nairobi hakuna hata mwafrika mmoja aliyesema naungana na Kenya kulaani na kuombeleza pamoja.
Tatizo wa Afrika bado hatuja jikomboa kifikra,bado tuna amini mambo yanayotokea nje ya bara la Afrika ni bora zaidi kuliko yanayotokea kwetu Afrika.Bado tuna ujinga fulani fulani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom