mawaso na unatamani iwe hivyo lakini ukweli ni kwamba hayo yote uliyotaja nayo yana shida sana baada ya kuchakachuliwa kwa kiasi kikubwa.
bahati mbaya mamlaka zilizo na nguvu ya kututetea ziko bize na siasa bada kufanya mambo kutuokoa wananchi.
tunakula sumu nyingi sana watanzania wenzangu,sasa hivi kila kitu kinapigwa dawa tena bila kuzingatia muda wa tangu kipigwe dawa hadi kifike kwa mlaji wa mwisho.
mfano mkubwa ni nyanya,matikiti,matango,karoti na mboga nyingi za majani...juzi nimeuziwa nyanya zikiwa na madoa meupe kabisa na harufu kali ya dawa ni kama zimetoka kupigwa jana yake zikaja sokoni,sasa unakula hizi unasema umekula salad natural kumbe umebugia sumu wazi wazi.
kama umewahi lima matikiti basi huwezi kuyala kabisa,mimi niliyalima,ule mchakato wake hadi linakua lile tunda kubwa limevimba jekundu ni mwendo wa madawa na kemikali mtupu,sisi tunakuja enjoy mchuzi ule na mtoa mada anasema kula kipande cha tikiti...bila kujua hilo tikiti limejaa sumu zilizotumika kulikuza,halafu unakuta mtu anakula matikiti yaliyokuzwa kwa madawa halafu anamcheka anayekula kuku wa kisasa,ujinga mzigo!!!
unasema mayai ya kienyeji eehh..kuku wa kienyeji siku hizi nao wanabugizwa madawa kibao,tofauti na wa kisasa labda kwenye vyakula tu,ila wanakula vyakula maalumu ili kuongeza rate ya kutaga,kwahiyo nao wamejaa madawa shazi tu...hapo ni tembea kwa kila kitu.
wizara ya afya sijui kama imeshaliona hili tatizo,hakuna kabisa control ya bidhaa gani za vyakula ziingie sokoni kwa vigezo vyake,kuna habari kuwa hata nyama buchani pamoja na samaki zinapigwa dawa za kuhifadhia maiti ili zisioze na wauzaji wasipate hasara,hakuna anayejali...sasa unakazana kusema unakula samaki natural kumbe keshapigwa kemikali kali za kutunza asioze,hakuna anayejali!!!!
kuna mdau juzi aliuliza kwanini siku hizi homa za ini na figo zinaua sana,vijana wadogo tu tayari wanaumwa figo na maini,sababu ni haya masumu tunabugia kila siku kwenye vyakula.
hakuna kitu natural tunakula zaidi ya vichache saaaanaaa... kwahiyo hakuna aliye salama.
ndio maana wenzetu wana utaratibu wa kupima kiwango cha kemikali kwenye vyakula.
organic farming is the only solution, otherwise tutazikana sana maniner..