Hii ndio dawa ya Clomiphene inayotumika kutibu uzazi kwa wanawake / Clomifene citrate

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
104
151
DAWA YA CLOMIPHIENE

Dawa hii hufahamika kama ‘Clomiphene Citrate’

Katika fani ya Tiba ya dawa, Clomiphene huwekwa katika kundi la dawa liitwalo ''ANTIESTROGENS AND SELECTIVE ESTROGEN RECEPTOR MODULATORS (SERMs)''

Kwanza kuelewa maana ya ‘ANTIESTROGENS ’ ni nini?
Hii ni dawa inayoleta upinzani dhidi ya kichocheo au homoni ya ‘Estrogen’ mwilini.

Clomiphene Citrate huzuwia homoni ya Estrogen Clomiphene Citrate ipo katika kundi la dawa zinazo zuia utendaji kazi na uzalishaji wa homoni ya Estrogen na kuzuwia athari au matokeo ya Estrogen katika mwili.

Hapo tumemaliza, tunakuja sehemu ya pili.
Nini maana ya SELECTIVE ESTROGEN RECEPTOR MODULATORS?

Clomiphene Citrate Hufanya kazi yake kwa kuzuia kipokezi cha homoni ya Estrogen, kikawaida kila homoni huwa ina vipokezi vyake katika mwilini viitwavyo (Receptors).

Sasa dawa hii ya Clomiphene Citrate hudhibiti kichocheo cha Estrogen kwa kuzuwia na kudhibiti kipokezi chake kiitwacho Estrogen Receptor.

Clomiphene Citrate huzuia au kukandamiza uzalishaji wa homoni ya Estrogen mwilini kwa kudhibiti vipokezi vya Estrogen ndio maana Clomiphene Citrate imewekwa kwenye kundi la dawa liitwalo ANTIESTROGENS AND SELECTIVE ESTROGEN RECEPTOR MODULATORS (SERMs)

Dawa ya Clomiphene Citrate inapotumika kwa mwanamke hufunga vipokezi vya homoni ya Estrogen kwa kuchochea tezi ya pituitary ndani ya ubongo, ndipo Clomiphene Citrate inaanzisha kuamsha uzalishaji wa homoni ya uzazi iitwayo Gonadotropin releasing hormone ambayo ni kidhibiti kikuu cha mhimili wa uzazi kwa mwanamke kinacho amuru uzalishaji wa homoni za aina mbili zifuatazo.

Moja wapo ni homoni ya Follicle Stimulating hormone FSH ambayo husaidia kudhibiti mzunguko wa hedhi na huchochea ukuaji wa mayai kwenye kifuko cha mayai (ovary).

Na homoni ya pili iitwayo Luteinizing hormone LH yenye jukumu muhimu katika maendeleo na utendaji wa kijinsia kwa mwanawake.

Luteinizing hormone LH husaidia kudhibiti mzunguko wa hedhi. Pia huchochea kutolewa kwa yai kutoka kwenye kifuko chake (ovary) baada ya yai kukomazwa kwa msaada wa homoni ya Follicle Stimulating hormone FSH

Hali hii sasa ya kutolewa kwa yai hujulikana kama kupevuka kwa yai (ovulation.)

1665864712824.png

Labda kabla ya kuendelea inatakiwa tufahamu kwanza hii homoni ya Estrogen ina kazi gani mwilini, hadi dawa ya Clomiphene Citrate ije kuidhibiti ili mwanamke apate ujauzito.

Kazi kubwa ya homoni ya Estrogen hutumika kudhibiti mzunguko wa hedhi.

Estrogen hufanya kazi katika njia ya uzazi, njia ya mkojo, moyo na mishipa ya damu, mifupa, matiti, ngozi, nywele, utando laini, misuli ya nyonga na ubongo.

Viwango vya juu vya homoni ya Estrogen vinaweza kusababisha dalili kama vile hedhi isiyo ya kawaida au kutokwa na damu nzito, kuongezeka uzito, uchovu, na kupatwa na uvimbe wa kizazi kwa wanawake.

Kwa wanaume, ongezeko la Estrogen husababisha ukuaji wa tishu za matiti kwa vijana wanao balehe au watu wazima, ugumu na tabu ya kudumisha msimamo wa uume na wakati mwingine uume kushindwa kusimama, na kupelekea utasa.

Viwango vya chini vya homoni ya Estrogen vinaweza kuingilia kati maendeleo ya kijinsia na kazi za tendo la ndoa. Inaweza pia kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na mishipa.

Kwa hivyo inapogundulika mwanamke hapevushi mayai kutokana na kiwango cha juu cha homoni ya Estrogen ndio hupatiwa dawa ya Clomiphene Citrate kwa ajili ya kusaidia upevukaji wa mayai kwa namna nilivyoelezea hapo juu.

NAMNA CLOMIPHIENE INAVYOTUMIKA
Clomiphene Citrate huchukuliwa kwa njia ya kumeza kwa mdomo, kisha hufyonzwa na kuingia kwenye tishu za mwili. Nusu ya nguvu ya dawa hii huchukua siku 6. Kwa kiasi kikubwa huchakatwa kwenye ini na sumu yake hutolewa kupitia nyongo (Hepato-biliary excretion) kisha huingia kwenye utumbo na kutolewa nje kupitia kinyesi.

MATUMIZI
Katika kutibu utasa unaosababishwa na ongezeko la homoni ya Estrogen

Clomiphene citrate hutumika kwa ujazo wa mg50 kila baada ya masaa kwa siku 5 kutoka siku ya 2-5 ya damu ya hedhi. (Walau itumike mizunguko 6 ya hedhi.)

AU

Ujazo wa mg50 mara moja kwa siku kwa muda wa siku 5,kuanzia siku ya 5 ya mzunguko wa hedhi. Matibabu hutolewa kila mwezi.

Mimba hutokea kwa wanawake wengi ambao hapo awali walikuwa hawapati hedhi ipasavyo au walikuwa na mizunguko ya hedhi isiyo pevusha mayai.

1665864863497.png

ORODHA YA MATATIZO YA KIAFYA YASIYO TARAJIWA YANAYO WEZA KUJITOKEZA WAKATI WA KUTUMIA CLOMEPHENE.

1-KUPATWA NA UVIMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI (Polycystic Ovaries)
Huu ni ugonjwa wa homoni unaosababisha kuongezeka na kuvimba kwa vifuko vya mayai kwenye kingo za nje za kizazi. Dalili ni pamoja na kuharibika kwa hedhi, ukuaji wa nywele kupita kiasi, chunusi na unene kupita kiasi.

2-MIMBA YA MAPACHA
Mimba iliyo na zaidi ya kijusi kimoja. Ikiwa zaidi ya yai moja yaliyopevuka na kurutubishwa wakati wa mzunguko wa hedhi, zaidi ya kiinitete kimoja kinaweza kupandikizwa na kukua kwenye mji wa uzazi.

3-KUONGEZEKA KWA JOTO LA MWILI (Hot Flash)
Ni hisia ya ghafla ya joto katika sehemu ya juu ya mwili, ambayo kwa kawaida ni kali zaidi juu ya uso, shingo na kifua. Ngozi inaweza kuwa nyekundu, kana kwamba unaona haya. Kiwango cha moto kinaweza pia kusababisha jasho. Ukipoteza joto la mwili kupita kiasi, unaweza kuhisi baridi baadaye.

4-KUTIBUKA KWA TUMBO (Gastric upset)
Kuhisi usumbufu wa sehemu ya juu ya fumbatio la tumbo, unaofafanuliwa kuwa na hali ya kuungua, kuvimbiwa au kutokwa na gesi, kichefuchefu au kushiba haraka sana baada ya kuanza kula.

5-KIZUNGUZUNGU (Vertigo)
Ni hisia kwamba wewe, au mazingira yanayokuzunguka, yanasonga au yanazunguka. Hisia hii inaweza isionekane kabisa, au inaweza kuwa kali na kushindwa kufanya kazi za kila siku.

6-MZIO WA NGOZI (Allergic Dermatitis)
Clomiphene Citrate huweza kusababisha mmenyuko wa kinga katika ngozi. Na mwisho kabisa dawa hii huweza kupelekea hatari ya kuongezeka kwa ukuaji wa uvimbe.

ONYO:
Epuka matumizi ya dawa za kujichukulia, hakikisha dawa zote unazo tumia umeandikiwa na DAKTARI. Kwani dawa nyingi ni sumu na ni hatari kwa AFYA YAKO ikiwa zitatumika ndivyo sivyo.
 
View attachment 2388485

View attachment 2388486

Dah asante sana kwa bandiko umenisaidia sana dawa hii nimeandikiwa hospital hata cjaanza kuitumia angalau nimejua ABC zake be blessed
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom