Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Matokeo ya Nape Nnauye ya Ordinary level secondary education ni Division TWO..,kwa anayetaka kujiridhisha anaweza ku-google mwenyewe NECTA matokeo ya Nsumba Secondary 1997. na hata kwa matokeo mengine pia ambayo Ni ya ndani ya Nchi na kuhusu matokeo ya chuo cha bangalore nayo yapo TCU.,ni jambo la kuuliza na kujibiwa.
 
tunataka aweke alama alizozipata A'level na O'level, hakuna aliyeomba CV hapa! aonyeshe masomo yake alifaulu vipi!
By the way nape yupo mbona mnaleta ukada hapa si aje mwenyewe? hata sisi ambao hatuna vyama tupo interested na kujua perfomance yake equally alivyokuwa anamponda mnyika!

weka na ya kwako tuone, mnyika alikwepa jibu akajitungia swali lake lingine kabisa akaamua kutoa historia ya maisha yake badala ya kueleza kiwango chake cha elimu
 
oie!
mnyika o'level kapata A tisa, A'level kapata division 11, mbona nape anakwepa kuweka credit zake?
 
weka na ya kwako tuone, mnyika alikwepa jibu akajitungia swali lake lingine kabisa akaamua kutoa historia ya maisha yake badala ya kueleza kiwango chake cha elimu
kama unashindwa kuelewa historia ya elimu na historia ya maisha una matatizo.
 
BUTIMBA TTC ni chuo cha ualimu lakini ni center ya kufanyia mitihani kwa wanafunzi ambao hawako mashuleni.,na hili ni kwa sababu Mheshimiwa Nape hakuwa ameendelea na sekondari kwa mtindo wa Boarding School.,kwa kuwa hakupenda kuendelea kukaa boardingi hivyo aliyasoma masomo yake ya high level akiwa nyumbani na kisha kwenda chuoni hapo kufanya mtihani wa form six.
 
Kumbe ni mwalimu wa elimu awali pale Butimba. Kwi kwi kwi! Ndo maana hata wazee wetu kanaona kama watoto
 
NO! NO! NO! NO!!! Usipotoshe jukwaa Ndg Nnape!!

TUNATAKA MATOKEO YAKO YA FORM FOUR NA SIX HAPA!! Sio blah blah!!

Diploma mwaka mmoja!!!
 
Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe
hapo ndio watu wanapodondokewa na kitu chenye ncha kali.. tunaomba na wengine mnapokuja na siasa za elimu zenu msisahau kuonyesha kipengele hicho yaani KIWANGO CHA JUU CHA ELIMU YAKO, HATA KAMA STD SEVEN NDIO MAJAALIWA YAKO
 
BUTIMBA TTC ni chuo cha ualimu lakini ni center ya kufanyia mitihani kwa wanafunzi ambao hawako mashuleni.,na hili ni kwa sababu Mheshimiwa Nape hakuwa ameendelea na sekondari kwa mtindo wa Boarding School.,kwa kuwa hakupenda kuendelea kukaa boardingi hivyo aliyasoma masomo yake ya high level akiwa nyumbani na kisha kwenda chuoni hapo kufanya mtihani wa form six.

acha kuzungukazunguka sema ALI "RESEAT" BAADA YA KUPATA 4 YA 29.
 
Nape ni msemaji wa CCM na Nape naye anamsemaji wake ndio huyo aliyeweka hiyo CV hapo so msishangae kwanini Nape hajaandika mwenyewe ilihali ni member humu, ni mgawanyo wa majukumu na wengine mkono uende kwa kinywa, ila hapo BUTIMBA TTC nadhani kijana unaweza ukawa _ fired nenda kajipange uje ufafanue vizuri.
 
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)

Naomba ufafanuzi wa hapo pekundu. Je ile DIV IV ilimpeleka Butimba? kusoma A level au Ualimu? Je anayo DIPLOMA ya UALIMU kutoka Butimba? au Butimba ni Sekondari?
 


  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu “3” kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu

Ukiona mtu anahamahama shule ujue kuna tatizo.....aidha la kinidhamu au la walezi/wazazi........halafu hii haina qualifications za kuitwa CV........imekaa kama ukle wasifu wakati wa mazishi ya mtu!
 
Tuanzie hapa form 4

NAPE NNAUYE
SEX M DIV IV PTS 29 KISW D HIST D GEOG D ENGL F B/MATH F BIOL D CHEM D PHY D CIV F
-----------------------
JOHN MNYIKA
SEX M DIV I PTS 7 PHY A CHEM A BIOL A CIV A ENGL A GEOG A HIST A B/MATH A KISW A B/KNOW A
 
Back
Top Bottom