Hii ndio Bei ya unga wa sembe na dona nilipo

Mchele ni gharama hata ukiwa bei sawa na unga. Ugali hauna viungo wala hautumii nishati nyingi. Wali lazima mafuta ya kula chumvi na sisi watu wa pwani lazima upaliwe na mkaa wa kutosha.... Sawa na kusema watu hawana mkate basi wale keki... Wafanyakazi wataumia zaidi coz kipato chao chote kitaishia kununua chakula. Huku wakulima vijijini wakila maembe na majani
 
Habari wakuu, hali ya maisha imezidi kuwa mbaya kiuchumia kwa baadhi ya raia wengi wa nchi hii. Pesa ikiwa haipatikani na ikipatikana hamna cha maana unachoweza kuifanyia...

Nimekuwa nasikia kupanda kwa unga tu, jana nimepita mashine kununua unga kilo 25 kwa bei ya jumla na kukuta unga umepanda bei kwa asilimia kubwa mwanzo unga kilo 25 tulikuwa tunanunua kwa sh.32.000 ila kwa sasa umefika sh 37000...

Bei ya reja reja kwa eneo nililopo kilo moja ni 1700.. Itakuwa vyema uzi huu ukatumika kupeana bei ya chakula hiki muhimu kwa watanzania wengi.
adfba84f3f18c8ee03dc844ec17d2a4c.jpg
e8ab08f50309bbc0f9692d43229857a5.jpg
019a2a868b6d355f5f05284cbc510966.jpg
Marufuku Nisisikie mtu anazungumza habari ya njaa wala ugumu wa maisha mpige kazi tu by MOBUTU SE SESEKO wa Tz
 
Habari wanajanvi!
Leo asubuhi nilienda kwenye duka la Mangi mtaani kwetu kununua sukari nikajiandalie kachai kangu ka asubuhi,ndipo Mangi akanambia kwamba hana sukari anajishauri kwanza kabla ya kufata mzigo, kutokana na hiyo bidhaa kwa sasa kupanda bei huko wanakonunua japo hajaniambia kwa kiasi gani imepanda,kwa kuongezea akasema pia na unga umepanda bei kwahiyo tutegemee bei mpya ya hizo bidhaa.Hakika sasa maisha yatazidi kukaza na inaonyesha serikali imeshindwa kabisa kutatua suala la sukari.
 
Mmmhh nkisikia ivi kale ka wimbo ka capt. Komba kananijia akilini.......
 
Hakuna ukweli wowote kwenye Uzi huu. Upuuzwe ( usimuamini mtu wa kaskazini kilaisi )
 
Leo nilienda maeneo ya ILULA-MAGU, MWANZA kununua pumba za Mahindi kwa ajili ya Mbwa na Bata nilikuta kwenye mashine ya kukoboa na kusaga Unga wananchi wananunua pumba za mahindi alafu wanazisaga kuwa Unga wa kupika Ugali. Pumba kisado kimoja TShs 1,500 na debe moja la pumba TShs 5,000 . Sado moja ya mahindi TShs 4,500 na debe la mahindi TShs 22,500!
 
Leo nilienda maeneo ya ILULA-MAGU, MWANZA kununua pumba za Mahindi kwa ajili ya Mbwa na Bata nilikuta kwenye mashine ya kukoboa na kusaga Unga wananchi wananunua pumba za mahindi alafu wanazisaga kuwa Unga wa kupika Ugali. Pumba kisado kimoja TShs 1,500 na debe moja la pumba TShs 5,000 . Sado moja ya mahindi TShs 4,500 na debe la mahindi TShs 22,500!

Kama ni kweli!! hawajui wanachokula ni sumu?
 
Back
Top Bottom