Hii ndio Bandari yetu dhidi ya washindani wetu

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Bandari yetu ya Dar es Salaam iliyopo Kurasini ndio bandari katika nchi yetu, na ni bandari ya pili kwa uwezo wa kuhudumia mizigo hapa Afrika Mashariki.

Bandari ya Dar es Salaam inawashindani wa kibiashara wakuu watatu kwa upande huu wa Bahari ya Hindi Kusini mwa Jangwa la Sahara. Washindani hao ni Mombasa Port, Kenya, Beira Port, Mozambique (Msumbiji), Durban Port, South Africa

Sifa ya bandari yetu dhidi ya bandari washindani. Dar es Salaam Port ina 11 (berths) pamoja na jetty ya KOJ1, KOJ2 Kwa ajili meli za mafuta na gas (LPG) na SBM kwa kule Mji Mwema Kigamboni kwa meli kubwa za mafuta na tuna lighter quay kwa ajili ya majahazi na Ferry Terminal kwa ajili ya boat za kwenda Zanzibar
tuna gati (berth) tatu tu maalum zinazohudumia meli za makontena.

Kina (draft) 11meters kwa KOJ na 15meters kwa gati 0-11, SBM Mjimwema ni 32meters (draft), Channel depth 15 meters.

Sifa za bandari washindani
1. Mombasa Port in Kenya
Bandari ya Mombasa ina gati (berths) 19 sita Kati ya hizo ni maalum kwa kuhudumia meli za makontena. KOT jetty ni maalum kwa meli mafuta na gas ( LPG). Draft depth 17.5 meters. Channel depth 55 meters.

2. Beira Port in Mozambique
Bandari ya Beira ina gati (berths) 11 nne Kati ya hizo ni maalum Kwa kuhudumia meli za makontena. Draft depth 12 meters. Channel depth 11 meters.

3. Durban Port in South Africa
Moja ya bandari kubwa Africa na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Bandari ya Durban ina gati 59 (berths) saba kati ya hizo ni maalum kwa kuhudumia meli za makontena. Draft depth 16 meters
Channel depth 19 meters. Upana 222 meters.

Ushauri wangu kwa serikali: Tuongeze idadi ya gati (berths) ili kuhudumia meli nyingi kwa wakati mmoja hivyo kutoa ushindani mkubwa kwa wapinzani wetu.
 
Back
Top Bottom