Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Leo kwenye uchambuzi wa magazeti radio one nimesikia kuna shule kibaha inawawekea alama nyekundu wanafunzi wenye vvu kwenye sale zao. Hivi,bado kuna unyanyapaa mpaka leo? Tukiamua kufanya namna hii, ni walimu,manesi,madaktari,wahasibu na watumishi wengine wangapi watawekewa alama? Hii kuambukizana kwa makusudi ni kwa sababu ya unyanyapaa,wangapi watarudi kwenye kuambukiza watu makusudi? Ni wangapi mpaka leo hatujapima na tunaendelea kutembea mtaani,na tutaogopa kwenda kupima?