Hii nchi ni huduma gani ya uhakika?

Hii nchi ni huduma gani ya uhakika?

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,630
Reaction score
11,096
Kwakweli kwenye sekta ya Teknolojia hasa huduma za kifedha hizi kampuni zinatia hasira sana.

Jana nimefanya muamala kwa T-Pesa (TTCL) kwenda HaloPesa (Halotel) haukukamilika, nikawapigia simu huduma kwa wateja, masaa 24 yamepita muamala haujakamilika na pesa haijarudi kwenye akaunti.

Leo nimefanya muamala kwenda Selcom Pesa: pesa ikafika vizuri tu ndani ya sekunde kadhaa. Hiyo pesa nilikuwa nataka kufanyia malipo mtandaoni kupitia Virtual card. Cha kushangaza wakati nafanya malipo yakawa hayakamiliki, kurudi kwenye app ya Selcom Pesa nakuta Virtual card niliyotumia mara ya mwisho mwezi uliopita tu imefutwa na natakiwa ku-request card mpya. Nime-request card mpya bila mafanikio, nikaamua kufunga app, cha kushangaza zaidi sasa hivi siwezi kuingia kwenye akaunti yangu.

Sasa ningependa kujua, nchi hii ni huduma gani inayotolewa kwa uhakika?
 
Mkuu huduma ya kupata kadi ya mpiga kura ni fasta sana tena unabembelezwa kabisa.
 
ingawa hii post ni muda kidogo, kwa upande wa selcom tumia plastic card yao, ipo vizuri. ni tsh 2500 tu.
 
ingawa hii post ni muda kidogo, kwa upande wa selcom tumia plastic card yao, ipo vizuri. ni tsh 2500 tu.
Hii plastic card unaipata wapi Na Je unaitumia kwenye sehemu Gani mana Kuna maeneo yana bank zile common tuu Sasa hio card itakuwaje
 
Hivi nani alikushauri kutumia TTCL kwenye huduma za kifedha?
 
Labda mwendokasi 😂😂😂

IMG-20250928-WA0048.jpg
 
Back
Top Bottom