Hii nchi imekuwa kama familia ya kambale, kila mmoja ana ndevu

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,031
3,911
Hii nchi yetu sasa imekuwa ya ajabu sana.

Viongozi wetu nao wamekuwa vituko na watu wa ajabu kabisa. Imekuwa kama familia ya kambale ambapo ukoo mzima una ndevu.Yaani kanchi kamekuwa na mambo ya kipuuzi puuzi tu yasiyokuwa na adabu. Kanchi sasa hakana mipango, hakana sera wala hakana uelekeo, kila mtu anajifanyia fanyia mambo anavotaka.

Vinatokea vijitu vya ajabu ajabu na kutoa matamko na maelekezo ya ajabu ajabu na kisha vinafikiri vyenyewe ni vijanja kumbe ni vipumbavu tu. Vinasahau kabisa kwamba hoja haifungwi gerezani wala haizikwi. Hoja inajibiwa kwa hoja na siyo vioja.

Taifa limekuwa kama choo cha stendi kila mtu anafanya chochote cha kipumbavu kama vile hakuna sheria. Kama mmeishindwa nchi mnafikiri mnaweza tenda miujiza? Hamuwezi.

Wafuatao sasa wataingia kwenye orodha ya kunyimwa kusafiri duniani. Ataanza Bulembo, kisha atafuatia Mama Lwakatare, kisha tafuatia Job Ndugai. Kisha World Bank watawalima ban za kutosha na IMF watafuata mpaka akili ziwakae sawa. Mnaongoza kanchi kipumbavu halafu mnataka watu wawangalie tu mkifanya ujinga wenu huo. Hakuna kitu kama hicho. Ni lazima mnyooshwe kabisa.

Sasa subirini bado mambo matamu yanakuja mpaka mtarudi huko mlikotoka.
 
Back
Top Bottom