Denicedion
Member
- Jan 11, 2015
- 33
- 7
Msomi mmoja mwenye PhD pamoja na kijana mmoja ambaye hakubahatikkusoma walisafiri pamoja kwenda kutembelea mbuga moja maarufu yenye maua na ndege wa kuvutia.Usiku ulipofika wakaweka hema lao zuri na la kisasa na wakalala usingizimzito kabisa.Masaa machache baadae,Yule kijanaasiye msomi akamuamsha yule msomi na kumwambia'hebu angalia angani.
Kisha niambie umegundua nini jamaa mwenye PhD akajibu."Naona mamilioni ya nyota na mbalamwezi.Yule kijana asiye msomi akauliza tena unajifunza nini ukiona hivyo msomi akatafakari kwa dakika kadhaa kisha akajibu."Upande wa kiunajimu inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi sana katika hii dunia kwetuwanadamu.
Upande wa muda inaonyesha ni usiku wa manane.Upande wa imani inadhihirisha kuwa Mungu ni muweza wa yote na sisi
kwake ni viumbe wadogo sana, na tusio na mamlaka.Upande wa hali ya hewa kesho itakuwa siku nzuri sana"PhD kisha naye akauliza,kwa upande wako wewe umegundua nini,yule jamaa asiye msomi akakaa kimya kwa muda na kisha akajibu:Nimegundua kua hema letu limeibiwa.