Hii Mikoa Nani Kailoga?

Hii Mikoa Nani Kailoga?

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,361
Reaction score
27,740
Habari za majukumu wana-Jf,.

Hapa nazungumzia mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara,.

Siyo jambo la siri mikoa hii ipo nyuma sana kimaendeleo au naweza kusema imesahaulika katika sura ya nchi yetu,.

Huwezi kulinganisha mikoa hii na mikoa mingine Tanzania kama Kilimanjaro, Mbeya na mingine ambayo imepiga hatua katika suala la maendeleo, uchumi na hata elimu,.

Nalitaka kujua kulikoni kwa hii mikoa kuwa nyuma katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo,.

Lengo la huu uzi siyo lingine zaidi ya kufahamu sababu za hii mikoa kuwa nyuma kwa hiyo mizaha na matusi hayatakuwa na tija katika kujuzana.
 
Kuna uzi humu unaomuhusu Forogo Ganze "master", mchawi alieanzisha mwenge, kapate maoni ya wadau. Kiimani zaidi.
 
Mtwara inakuja kwa speed kubwa sana,siyo ya siku zile tena...itafunika mikoa mingi tu muda si mref...just a matter of time.
 
Mtwara inakuja kwa speed kubwa sana,siyo ya siku zile tena...itafunika mikoa mingi tu muda si mref...just a matter of time.

Unazungumzia hapo Mtwara mjini? Nenda huko vijijini mkuu huwezi amini kama uko Tanzania.Umasikini unatisha!
 
Mikoa hiyo imerogwa na ccm ila Lindi na Ntwara zitachomoka maana wamejua maana ya upinzani. Hakika Ruvuma kama mtaendelea kuwachagua Jenister. kaka Komba na Kawawa mnapaswa kuhurumiwa. mtabaki huko huko nyuma kwenye mkia
 
Mtwara inakuja kwa speed kubwa sana,siyo ya siku zile tena...itafunika mikoa mingi tu muda si mref...just a matter of time.

Sielewi mwansisha mada na wachangiaji wengine wako ulimwengu huu ama ahera...Mtwara unaiweka kundi la mikoa duni ?tena kwa nyakati hizi....Hahahaaaaa, inafurahisha!! Macho na masikio ya serikali yetu hii na dunia nzima yanaelekezwa Mtwara...Ujeuri wa viongozi wengi sasahivi ni kwasababu ya Mtwara...
"Mtwara Kuchele"
 
Tz hakuna sehemu ambako ni hafadhari ndo mana ktk majiji 200 bora hakuna jiji 1 la Tz musijipe moyo na dar,arusha na mwanza yote ni hovyohovyo tembeeni muone miji watu ilivyo
 
Tz hakuna sehemu ambako ni hafadhari ndo mana ktk majiji 200 bora hakuna jiji 1 la Tz musijipe moyo na dar,arusha na mwanza yote ni hovyohovyo tembeeni muone miji watu ilivyo

kwa hapa Tz mikoa hii bado ipo nyuma mkuu ukilinganisha na mingine,.
 
Naungana na wewe katika hili!!

Nilikua sijatembelea mikoa ya kusini. Ni majuzi tu nilipata safari ya kutembelea Lindi na Mtwara,,,

Sikuamini macho yangu nilipofika Lindi mjini,,,da,,yaani pamechoka balaa,,hadi nikawa nauliza mara mbili mbili,,jamani hapa ndio Lindi?

Mtwara afadhali kidogo kuliko lindi,,japo na penyewe ni choka tu,,,hiyo mikindani inayovuma kihistoria,,panasikitisha,,,nyumba zimeshoka kinoma,,,aisee!!
 
Back
Top Bottom