Hii mikakati iliishia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii mikakati iliishia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bubu Msemaovyo, Nov 24, 2008.

 1. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Katika awamu ya Tatu, tulikuwa na mikakati mingi kama ifuatayo: Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA), Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara kwa Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Mkakati wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES), Mkakati wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).Mikakati ilikuwa na malengo mazuri na yenye nia ya kuendeleza nchi yetu. Katika miaka ya karibuni, sijasikia tena mikakati hii kuongelewa. Je, Mikakati bado hipo? Imefikia wapi? Je, awamu ya Nne iliichukua mikakati hii na kuiendeleza au ndio imeshatupwa kapuni?
  Mdau
  Dr Faustine


  Mkuu; Faustine
  Mkakati mwingine unaitwa MKUMBITA kirefu chake sikijui, wanaokijua wakimwage hapa.
   
 2. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #2
  Nov 24, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Awamu hii wanakazia sana Mkakati Wa Kukuza Uchumi Binafsi (MKUKUBI)
   
 3. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha,

  Hii forum kwa kweli ina mambo.

  Mkumbita na mkukubi ni kali ya yote.... Naona karibu watakuja na LAWAKWATA....

  Laumu
  Wananchi (wapinzani?)
  Kwa kila
  Tatizo
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahahah hii inaburudisha na kufurahisha, umefikiri nini mkuu LAWAKWATA
   
 5. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefikiria kinachoendelea sasa hivi Tanzania - Migomo ya walimu, migomo ya wanafunzi, migomo ya wazee wastaafu, bei juu za vyakula na usafiri, ukosefu wa ajira kwa wahitimu, na mengine mengi......

  Kisha nikafikiria majibu yanayotolewa na watendaji wa serikali......

  Hakuna mtu anayekubali makosa au kuhusika kwake na ugumu wa maisha ya watanzania. Wengi wanasema kuwa ni makosa ya wastaafu, walimu, watoto, wanafunzi, au/na labda kuwa ni juhudi za wapinzani kuipaka matope serikali.

  hence..... LAWAKWATA......
   
 6. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkakati wa Kupambana na Migomo Tanzania nao kwa kifupi utaitwa MKUMITA
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Nov 25, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sina hakika kama muuliza swali ameuliza kiutani au la. Kama ni kiutani basi majibu yaliyokwishatolewa yanatosha. Kama sio kiutani basi majibu ndio haya hapo chini japo muuliza swali itabidi akafuatilie kwa undani kwenye tovuti za mikakati/mipango hiyo kwa maelezo zaidi:

  Mkukuta/NSGRP ni 'Mkakati Mama' unaoongoza mipango yote ya nchi, ulianza 2005 unaisha 2010 ila kwa kawaida huwa unaongezewa muda na kubadilishwa muundo wake maana hata kabla ya 2005 ulikuwepo kwa jina lingine la 'Makaratasi ya Kupunguza Umaskini'!

  Mkurabita/PBFP ni Mpango ambao kinadharia uko chini ya Mpango Mama wa Mkukuta; huu ndio kwanza unaanza maana toka 2004 walikuwa wanafanya utafiti na majaribio tu - sasa wako wilaya 10 wanaanza kuutekeleza baada ya majaribio ya Handeni, Hannanasif, Mbozi na Bagamoyo!

  Mkumbita/BEST huo nao ndio kwanza unaanza kupamba moto maana wafadhili wameumwagia pesa sana hasa ukizingatia kuwa maana yake ni Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania; haya mambo ya kulegeza masharti, kurahisisha usajili na kuweka vivutio ndio mambo ya BEST hayo!

  MMES/SEDP na MMEM/PEDP kawaulize HakiElimu maana wamekuwa wakiifuatilia kwa karibu sana, awamu ya kwanza ya MMEM iliisha 2006 na sasa wako awamu ya pili ila nadhani hauisikii sana kwa kuwa pesa hazijamwaga sana kama wakati ule wa Mungai - MMES haikupata ufadhili wa haraka na uhakika ndio maana sio maarufu sana kama ilivyokuwa MMEM; kilichobaki ni kujenga sekondari za kata na kutumia walimu wa voda fasta!
   
Loading...