Hii Mapambano Tuition Centre mmhh..!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,092
21,773
Habari za leo wakuu,

Mida flani hivi ya asubuhi bimkubwa aliniomba nikamlipie king'amuzi cha Star times pale Bamaga, basi nikaenda nikalipia fresh.

Wakati wa kurudi nikasema acha nipige andha kanoon (kutembea kwa miguu) hadi Mwenge. Basi nilipofika pale Nakiete building nikashawishika kukata ile kona niende Mapambano kumpa hai ndugu yangu bw. Mussa Biteba.

Ebwana eeeh, hii sio twisheni tena ni kama sehemu ya kabiashara fulani haramu na kituo cha vijana kuuza sura. Nilipishana na mabinti kadhaa eti ndo wanaingia pindi, dressing code nikajikuta kimoyomoyo nasema 'mayo nene nacha', nguo za kuvaa night clubs tena uwe na guarantee ya usafiri binafsi watoto wa kibongo ndo wametinga wanazama kubukua.

Ikabidi nisimame pembeni ni observe, kidogo ndo balaa likatinga, ebwana huyo sister kavaa kimini dzain hata akiangusha kalamu class hawezi okota kabisa, pembeni yuko na sijui ndio boy wake yule kavaa zile suruali wanapenda kuvaa wakongoman zile katikati linakua kama umejinyea hivi linatepweta.

Nikakumbuka enzi zetu za kwa hidden mchikidown, kwa Mbuge.. Nikasema kweli this is new school, I am way too old school (nikakumbuka msemo wa Danny glover kwenye lethal weapon akimwambia Mel Gibson 'am too old for this shit....').
 
Teh teh hiyo Suruali anakuwa kama vile kajinyea inaitwa Balotel. Halafu hao wanaorudia mitihani na QT wapo kama vile wamelogwa maana upumbavu ule ule uliowafanya wafeli wakiwa full school ndio wanaurudia tena kwa kasi ya ajabu kabisa.
Duuuh, ndo balotel? Daah kweli
 
Back
Top Bottom