Hii Logic ipo sahihi..?

Tunaweka katikati ya miji ili sadaka ziwe nyingi.
 
Umeeleza vizuri.
 
Nimewasoma vizuri ila kama vile kuna vitu siwaelewi au nina sababu za kupingana na ninyi.

Kwanza Wajerumani (Germans) na Ukatoliki wapi na wapi?

Ninachojua Wajerumani waliotawala Tanganyika kabla ya Waingereza walianzisha Makanisa ya Lutherans na ni kweli kuwa walijenga makanisa na ofisi KATIKATI ya miji/ majiji lakini kwa wakati huo ilikuwa ni miji midogo sana.

Ndio maana ukienda Dar es salaam, Moshi na Arusha kuna LUTHERAN CENTERS kwa DSM ipo Posta, Kwa Moshi ipo close na Stand Kuu, kwa Arusha ipo close na Clock tower na kwa Mkuu wa mkoa.

Majengo yote hayo imara yalijengwa na Wajerumani kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na bado yanatumika na kuonekana na ubora mkubwa sana.

Makanisa ya Roman Catholic na Lutheran yapo mijini kabisa mifano umeshatoa...kwa Moshi KKKT kanisa kuu lipo close na stand na RC pia pale Kristo Mfalme.

Kwa Arusha KKKT kanisa kuu lipo mjini kabisa karibu na Clock Tower pale Meat King, na la RC yaani St. Theresia pia lipo karibu kabisa na la KKKT, ni makanisa yanayotenganishwa na Mto unaotiririsha maji katikati ya jiji la Arusha tangu enzi.

Kwa Dar es Salaam tazama Azania Front ilipo, tazama St. Joseph RC church Zanzibar lilipo.

Yaani tangu 1861 ndio makanisa yalianza rasmi kushamiri kwa misheni ya Berlin kule Rungwe, Dsm mpaka Lwandai Tanga na Misheni ya LEIPZING ndio ilikuwa Uchagani na ikajenga makanisa, shule na hospitali kama KCMC

Kwa Zanzibar ndio kabisaa Wareno ndio waasisi wa ukatoliki tangu miaka ya 1400 alipokuja Vasco Da Gama kabla ya ujio wa waarabu na walijenga kanisa kubwa sana Mjini kabisa

KUHUSU MAKABURI

Kwa Lutherans kwa kawaida Marehemu anazikwa kichwa kikiangalia Mashariki jua linapochomoza yaani USO wake unatazama jua sio opposite kwahiyo msalaba unakuwa nyuma ya kichwa chake.

Na Makaburi yote ya Walutheri yapo hivyo dunia nzima hata Ujerumani kwenyewe, Sweden, Denmark etc

Kwa Wakatoliki sina uhakika ila najua kuwa Padri na Papa wanazikwa sawasawa na mwelekeo wa mathabahu (Altari)

Ujenzi wa makanisa haya yalizingatia zaidi vitu vya msingi sana katika maisha na hawa Wazungu walikuwa na Maarifa makubwa sana tangu zamani, kwa mfano walizingatia Idadi ya watu na jinsi watakavyoongezeka, accesibility ya barabara, Maji, Nishati ya Umeme n.k

Hata Makanisa, Shule na Mahosipitali waliyojenga mpaka leo hii ni ya standard ya juu kuliko majengo yetu ya karne hii.

Kama kuna swali tunaweza kusaidiana kujibu.
 
Sorry braza mimi nilijikita sana na conspiracies za wajerumani sio specifically na subject of the original post! Hayo mambo ya makanisa kujengwa katikati siwez kusema lolote zaidi ya kuona personally nayo kama conspiracy tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…