Hii Logic ipo sahihi..?

Jiulize jambo,wakati yanajengwa ilikuwa katikati ya mji?,rudi nyuma miaka hiyo yanajengwa
 
I am not sure kama ulichosema kama mfano kuhusu Rombo na Old Moshi kama ni sahihi mkuu. Sidhani kama Moshi Mjini ilipitwa kimaendeleo na Rombo na Old Moshi. Mimi nimefika kote huko lakini kwa mtizamo wangu nauona Moshi ni mji wa zamani zaidi kuliko Rombo na Old Moshi hata sio mji kamili ni maeneo tu ya kawaida (vijijini). Hapa watanisahihisha wengine (hiyo ni kwa experience yangu maeneo hayo).

Kuna vigezo vingi vinavyo determine location ya mji/jiji (city center). Zipo ishu za hali ya hewa, idadi ya watu, topography n.k. so mkuu nadhani pia hao missionaries wali consider hivyo vitu kabla ya kujenge hayo makanisa.

The most likely reason ni demographics. Isingekuwa rahisi kujenga kanisa kubwa sehemu ambayo pana wakazi wachache. So still naimani kuwa sababu sio kuwa walijua ndio katikati ya mji 'geometrically' bali ni sababu za ki demography na geography.
 
Jiulize jambo,wakati yanajengwa ilikuwa katikati ya mji?,rudi nyuma miaka hiyo yanajengwa
Katikati ya mji simaanishi kwamba ile Sehemu iliyoendelea zaidi bali vipimi vya kijeografia vinaonyesha pale ndio center ya mji. Sio kwa kuzingatia kuendelea kwa mji hapana.
 
Rudia tena kujiuliza kama vipimo vya eneo mfano la jiji la dar mwaka hilo kanisa linajengwa ndo hivihivi na havipanuliwi kiasi useme unaongelea eneo kijiografia siyo majengo
 
Rephrase please...


dunia hii ina mambo mengii sanaa. Mfano katika ujenzi wa haya majumba ya ibada ya imani mbalimbali uzijuazo, huwaga kuna vitu havikogo sawa tukianza na majumba yenyewe yapogo align toward direction fulani, na tunaweza sema vipo kawaida ila vinasababu ya kuwa vilivyo. vipimo vya ramani yake pia vipo kimafumbo, mavazi wavaayo hao waongoza ibada na ranks zao huwa zinatofautiana.
 
Nasikia enzi za Mwalimu kile kijijengo kilichochoka cha freemanson cheupe pale posta karibu na benki kuu, palitakiwa pajengwe kitu fulani kikubwa cha serikali, watu wa serikali wakamfuata Teacher wakamuuliza vipi mzee tuvunje ile hall akasema hapana msibomoe na wala msifikirie kufanya hivyo, kumbuka teacher hakuwahi kusikika alikuwa mwanachama na kama mnavojua freemanson ni NGo lakin lile jengo halikuvunjwa na wala kuwa nationalized. Therefore kuna mambo ni dogma.
 
Hivi uzi za aina hii ndo huwa mnaziita... Sijui ma introverts au extroverts...

Ni nini kwani hasa;!?
 
Cathedral Tanzania ipo moja, Bukoba
 
Miji yenyewe hiyo iliimarishwa na wamisionari na wakawa wanajiwekea huduma muhimu za kijamii zote ziwe karibu sasa kukiwa na kanisa unashangaaje tena!?

Tukirudi nyuma kidogo kwenye History ya ordinary level unasoma kabisa kuwa jamaa walitenga maeneo rasmi kwa shughuli zao na baada ya wao kuondoka ndipo unaona hadi leo yale maeneo waliweka makazi yao utakuta hayo makanisa

Ninakuongezea ili ukachunguze tena... utakuta pia shule kongwe, zahanati na huduma nyingine ambapo utasikia wabongo ile ni ya MISHENI

Sababu kubwa ni kwamba wale (hao) jamaa elimu ya mazingira (circular) wameibobea kabla yetu kwahiyo hata hayo maeneo waliyachagua si kwa kubahatisha bali waliconsider vigezo vingi hivyo mbongo huna uwezo wa kupaepuka kupaendeleza kukawa mji (yaani kunakuwa na sifa na vigezo vyote vya watu kupakimbilia)
 

Mambo mengine huwaga unaweza dhani ni stories lakin ndivyo yalivyo.
 
Kuhusu kuzika huzingatia
1.Kama ndani ya kanisa altare/madhabahu imekaaje mwelekeo.
2.Nje huwa tunazingatia eneo ni tambarale au mwinuko,jiografia ya maziko hujieleza kukwepa maji ya mvua isihamishe makaburi.mashariki/magharibu hakuna hiyo.
 
Unajua kuna muda nikikaa nikifikiria mambo ambayo Germany imepitia na conspiracies zao nabaki naogopa, kuna muda nawazaga inawezekana Yesu alikuwa some immortal sumerian amabaye alishinikizwa kukubali mateso na uongozi wa dynasty yake ili aje kuwa long loved and cherished public figure ila nakataa, sometimes nafikiria yawezekana Yesu alikuja in body of Hitler ili kurevenge kwa Judes kwa walichomfanyia ila nakataa, nikifikiria jinsi Germany ilivyoinvolve kwenye long recognized and deadly wars nabaki natetemeka, hizi conspiracies ninazosikia kuhusu artifacts ambazo wajerumani waliziacha baada ya vita ndio naogopa kabisa, mjeruman huyu huyu alimpiga Brazil nguli wa mpira tangu dunia iumbwe goli saba bila huruma kombe la dunia mwaka nimesahau, juzi kati nilikuwa naangalia series moja inaitwa "Dark" imekuwa produced huko huko ina theme ya time travel, jamaa hawaamini katika Mungu kabisa.
Pia kuna conspiracies nyingi tu zilikuwepo wakati wa holocaust huko Germany, huko kuna mambo mazito yawezekana, yawezekana huko kweli kuna wormhole!
 
Bwana Kit Harrington, ni bora umletee screenshot ya definition ya "cathedral" kutoka Google
Nimemkatalia huyo mdau alichosema maaa yale majimbo mauu ndio Cathedral yenyewe. Kwa Tanzania kuna Cathedral kama 22 kila mkoa ukiondoa mikoa iliyoanzishwa maybe miaka 20 iliyopita

Btw hoja zingine nitazijibu panapo majaaliwa
 
Nimemkatalia huyo mdau alichosema maaa yale majimbo mauu ndio Cathedral yenyewe. Kwa Tanzania kuna Cathedral kama 22 kila mkoa ukiondoa mikoa iliyoanzishwa maybe miaka 20 iliyopita

Btw hoja zingine nitazijibu panapo majaaliwa
Samahani hebu weka vizuri, umesema cathedrals 22 kila mkoa au umemaanisha 22 Tanzania nzima?
 
Makanisa ndiyo chimbuko la miji uliyoitaja, wazungu walipofika walijenga makanisa na ofisi zao na miji ikaendelezwa kuanzia hapo.
 
City centre ipi tz haina msikiti? Hizo sehemu zilikuwa na wakazi kitambo zats y zikatengenezwa nyumba za ibada
 
Kuna maandiko yanasema teache hakuwahi kuwa mwanachama wa freemason japo alijua wapo na hakutaifisha mali zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…