Hii Kweli-NZI wa Bongo waleta vioja!

Sura-ya-Kwanza

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
566
10
Katika pita pita yangu nilikutana na jamaa mmoja ambaye alipata hudhuriwa na Dada mmoja huko U es Of Ey---Siku ilikuwa nzuri na Stori za Bongo na hata za U es of Ey...Ikafika saa za kula, na wakati wa kula huyo Dada mmoja akaanza kuonyesha vituko ambavyo vilimfanya huyu jamaa wangu kushikwa na butwaa, akifikiri kuwa dada huyo ameengiwa na mashetani...:eek:


...Ilikuwa hivi, wakati dada huyo akila alikuwa anatupa mkono wake wa kushoto kama vile anaashiria, hajali-ondoka-toka-we mpuuzi-ugh,N.K
Jamaa wangu kijasho kinamtoka manake hajui kinachoendelea-lakini akajivuta kiume na kumuuliza kinachomsibu dada huyo-Dada huyo naye bila kuelewa jamaa anamaanisha nini akajibu, 'poa tu'- Butwaa hilo likaendelea kwa vijisekunde na ndipo alipouliza, Kwanini unatupatupa mkono hivyo?

Jibu lililotoka kwa dada huyo siyo tu lilimshangaza jamaa bali alianguka kicheko!

'Tumezoea kupepea NZI wakati tunakula sasa ni mazoea' alisema dada huyo!
:D:D:D:D

Inaonekana sasa hapa deezeem NZI kibao! or Atleast wanaanza kuleta vitabia vipya kama kutupa mikono hewani na kuwashangaza wenyeji wao huko Ughaibuni!

Mimi niliona hii kali kama siyo Kula Breki!!!
 
Inawezekanaje? Ugonjwa wa akili utakuwa huo sio kawaida sehemu hakuna NZI na uwe unawafukuza kwa kutupa mikono duuh
 
Back
Top Bottom