Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,471
- 23,744
Habari! Mimi nmejenga sehemu moja hapa Dar kms 16 kufika Posta kwenye Mnara wa Askari. Nachelea kusema ni mbali na Jiji au si mbali sana.
Kiwanja nilinunua kikubwa sana.of course Mzee alitununulia miaka hiyo ya 90s then nami nikaja ongezea so nina eneo la kutosha hasa. Nmejenga na nimepata sehemu ya kupanda miti miwili mitatu ya matunda.
Nina migomba, michungwa,miembe mbegu fupi,makoma manga,mipapai mbegu fupi na migomba.
But pia nina kaeneo ka bustan so wanalima kiasi mboga mboga na mapassion.
Eneo lote nimezungushia.nmezungushia kwa ukuta mrefu sana na kuacha kidogo tu kwa mbele ili kupitisha hewa.
Shida inayonifanya nianze kuchukia hapa home ni wadudu. Nimeshaambiwa mara mbili pameonwa na kuuliwa nyoka wa kijani.
Mimi ni NYOKAPHOBIA na WADUDUPHOBIA. Nipo tayari kupambana na mbwa lakini si wadudu.
Nakumbuka mwaka flani nikiwa chuo nlienda panga sehemu moja Msewe ukipita lile gate la Chuo kama unaelekea Changanyikeni. Nlihama ndani ya mwezi mmoja nikaacha chumba na kodi sababu ya uwepo wa Tandu na Nge wengi eneo lile.
Nlijikuta nashindwa kulala au kukaa room.sikuwa na amani kabisa.nlitafuta dawa nyingi mpaka nilikuja pata flani ambayo kidogo nami iniue.ile dawa ilikuwa unapulizia. Sikuwa nimeziba pua.ilikuwa ina hewa kavu na yenye kukaba kiasi kwamba ukipuliziwa ndani ukafungiwa unakufa.ilikuwa kavu sana na inakata pumzi huwezi vuta.
Nikaamua kuhama. Mimi binafsi hata mende mkubwa akiwa room kama hajatolewa (sipendi auliwe ndani) siwezi lala. Au nimwone mjusi wale wanaopenda kukaa ndani.siwezi pata amani mpaka atolewe (na sipendi auliwe pia)
Hili tatizo sielewi maana ikinyesha mvua hata kumbikumbi sipendi waniguse.napata shida sana. Kifupi sipendi mdudu yoyote around me.
Nyoka hata awe amekufa sipendi mwona au itokee nimguse.sipendi nyoka awe wa rangi yoyote ile.mweupe,mwekundu,njano,kijani au blue. Ni kwamba sipendi nyoka.
Lakini ukinambia kuna sehemu kuna mbwa mkali huyo wala haniogopeshi.nimetembea porini kwenye wanyama wakali sana na wakutisha sikuwa naogopa hata kidogo.ila nambie tu kuwa room kwao nmeona nge au tandu. Sitolala mpaka apatikane atolewe.
Nimeshawahi kimbiza fisi porini mara mbili nikiwa na panga,nmewahi kimbiza duma nikiwa na panga na mkuki. Lakini siku hiyo nmemkimbiza duma nmerudi kwenye tent jamaa yangu akasema amemwona mjusi kafiri kaingia kwenye tent yangu sikufunga vizuri zip. Sikulala.
Najaribu kuwaza nifanye nini kuepukana na hali hii ya kuogopa wadudu lakini pia kwa hapa home nazuiaje kabisa nyoka na wale mijusi wasikanyage kabisa home. Maana naanza kukosa amani.na binafsi sipendelei kwenda ishi kwenye maghorofa kule upanga,mikocheni n.k