Hii kwangu imekuwa changamoto kubwa. Hata natamani kukimbia home

😳😳😳😳😳 tandu kitandani? Hicho chumba ntapata wakati mgumu kushawishiwa kulala tena. Hao wadudu nikimwona tu mwili unasisimka. Napoteza sana.

Kama umezungushia ukuta ni vzr.. chukua Oil chafu.. mwaga chini kuzunguka nyumba.

Pili Tumia Dawa kali ya Fumigation puliza miti na vichaka vyote.

Unaogopa mende... Hehe last week nilivyokuw MAPORINI nimelala na TANDU mweusi kitandani kilichonishtua ni zile sharubu zake alikuw ananigusa gusa maskioni.. nikawasha Taa nilizan ni mdudu tu wa Kawaida nikamkuta Tandu.. so ni vitu vya kawaida.. hapa kwenyewe nishaua KENGE.. mdg lkn alikuwa anasumbua sumbua nje.
 
Nyoka wa kijani hangati kutokana na maumbile ya meno yake, hana meno kwa mbele, meno yake yameanzia katikati ya taya, hivyo kungata mpaka umkanyage na ahangaike kutoka
Anang'ata mkuu hata kama hujamkanyaga ila tu sumu yake sio tishio kama wengine.
 
Nikaamua kuhama. Mimi binafsi hata mende mkubwa akiwa room kama hajatolewa (sipendi auliwe ndani) siwezi lala.

Mbombo ngafu naloli...we ni mwoga tu jamaa...utotoni tumechezea sana wadudu..hawa vyura wadogo..wanakuwa na kimkia wanafanana na samaki (kambale) tumewala sana...tumekula mpaka panzi wa kuchoma....duh kweli kuna ntu na ntu..!!!
 
Kwa wanaime wa Daslam sikushangai mkuu, maana mnaogopa sana mende, mijusi, kumbikumbi, jongoo, kinyonga nk:
Maana hata wale wanyama wakali ambao mnajiamini hamuwaogopi, hua mnawaonea kwenye movie tu...
 
Nyoka wa kijani hawanaga madhara,unaweza lala nae ktandani,tuliwah ishi mahala walkuwa weng sana lakin hawakuwah kuleta madhara mwanzo tuliwauwa sana kwa sku tulkuwa tunaua watatu mpaka watano,jamaa mmoja akatueleza kuwa waacheni tu hawana shida mpaka Leo Mimi kama nyoka hayupo ndani hata kama ni wale weusi siwezi kumuua ni dhambi pale hajafanya kosa lolote why umuue
Usimdanganye kuwa nyoka wa kijani hana madhara. Inategemea ni nyoka gani kwakua nyoka wa kijani wapo wengi ambao ni venomous kama Green Mamba, Boomslang n.k

Lakini pia wapo wengine ambao ni nonvenomous.

Kikubwa mara nyingi nyoka sio rahisi ku attack mtu kama hajafeel threatened, yani simply mpaka nyoka akung'ate ni katika jitihada za kujilinda kama amehisi atadhurika.

Chamsingi watu msiue nyoka kama yupo nje mzuie tu asiingie ndani na kama yupo ndani mtoe nje mpeleke machakani huko usimuue.
 
Huku niliko kwangu kuna nyoka sana na kupambana nao ni jambo la kawaida, nilishawahi kung'atwa na kisa nikaleta humu.
Kuna majoka ya kila aina haipiti wiki lazima uwaone au uwaue wawili watatu na mpaka juzi saa moja usiku tumeua joka lenye unene wa tyre ya gari likitoka maeneo yangu na wenyeji wa huku wanaliita Bafe na kusifu kuwa ana sumu kali sana hivyo huua haraka sana.
Mazingira yeyote yanapokutokea usiogope bali jenga ujasiri! Mimi hadi hapa nilipo sasa hivi nimepumzika hapa ndani lakini najua kama sio chini ya kitanda basi nyuma ya makabati kuna nyoka, maana kila baada ya muda nakuta gamba nene jeusi lililo vuliwa na nyoka.


Hapo ningehama Mimi, nyoka hata nikiona kwenye tv tu, ninaogopa Sana, na nikilala lazima niote
 
Habari! Mimi nmejenga sehemu moja hapa Dar kms 16 kufika Posta kwenye Mnara wa Askari. Nachelea kusema ni mbali na Jiji au si mbali sana.

Kiwanja nilinunua kikubwa sana.of course Mzee alitununulia miaka hiyo ya 90s then nami nikaja ongezea so nina eneo la kutosha hasa. Nmejenga na nimepata sehemu ya kupanda miti miwili mitatu ya matunda.

Nina migomba, michungwa,miembe mbegu fupi,makoma manga,mipapai mbegu fupi na migomba.

But pia nina kaeneo ka bustan so wanalima kiasi mboga mboga na mapassion.

Eneo lote nimezungushia.nmezungushia kwa ukuta mrefu sana na kuacha kidogo tu kwa mbele ili kupitisha hewa.

Shida inayonifanya nianze kuchukia hapa home ni wadudu. Nimeshaambiwa mara mbili pameonwa na kuuliwa nyoka wa kijani.

Mimi ni NYOKAPHOBIA na WADUDUPHOBIA. Nipo tayari kupambana na mbwa lakini si wadudu.

Nakumbuka mwaka flani nikiwa chuo nlienda panga sehemu moja Msewe ukipita lile gate la Chuo kama unaelekea Changanyikeni. Nlihama ndani ya mwezi mmoja nikaacha chumba na kodi sababu ya uwepo wa Tandu na Nge wengi eneo lile.

Nlijikuta nashindwa kulala au kukaa room.sikuwa na amani kabisa.nlitafuta dawa nyingi mpaka nilikuja pata flani ambayo kidogo nami iniue.ile dawa ilikuwa unapulizia. Sikuwa nimeziba pua.ilikuwa ina hewa kavu na yenye kukaba kiasi kwamba ukipuliziwa ndani ukafungiwa unakufa.ilikuwa kavu sana na inakata pumzi huwezi vuta.

Nikaamua kuhama. Mimi binafsi hata mende mkubwa akiwa room kama hajatolewa (sipendi auliwe ndani) siwezi lala. Au nimwone mjusi wale wanaopenda kukaa ndani.siwezi pata amani mpaka atolewe (na sipendi auliwe pia)

Hili tatizo sielewi maana ikinyesha mvua hata kumbikumbi sipendi waniguse.napata shida sana. Kifupi sipendi mdudu yoyote around me.

Nyoka hata awe amekufa sipendi mwona au itokee nimguse.sipendi nyoka awe wa rangi yoyote ile.mweupe,mwekundu,njano,kijani au blue. Ni kwamba sipendi nyoka.

Lakini ukinambia kuna sehemu kuna mbwa mkali huyo wala haniogopeshi.nimetembea porini kwenye wanyama wakali sana na wakutisha sikuwa naogopa hata kidogo.ila nambie tu kuwa room kwao nmeona nge au tandu. Sitolala mpaka apatikane atolewe.

Nimeshawahi kimbiza fisi porini mara mbili nikiwa na panga,nmewahi kimbiza duma nikiwa na panga na mkuki. Lakini siku hiyo nmemkimbiza duma nmerudi kwenye tent jamaa yangu akasema amemwona mjusi kafiri kaingia kwenye tent yangu sikufunga vizuri zip. Sikulala.

Najaribu kuwaza nifanye nini kuepukana na hali hii ya kuogopa wadudu lakini pia kwa hapa home nazuiaje kabisa nyoka na wale mijusi wasikanyage kabisa home. Maana naanza kukosa amani.na binafsi sipendelei kwenda ishi kwenye maghorofa kule upanga,mikocheni n.k
Kuhusu kuzuia nyoka kuja kwako onana na Mama Diamond ama Muha yeyote wa Kigoma, wale ni wachawi wa asili na wanajuwa kuishi na hao wadudu.
 
We jamaa hii kama ya kufunga ngamia.

Umetembe wapi pori lenye wanyama wakali ukakosa mjusi, nyoka, na wadudu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom