Hii kwako unaichukuliaje?

Hii kwako unaichukuliaje?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,136
Reaction score
55,605
Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa. Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​
 
Ni ngumu sana wazazi kuomba binti yao aende kuwasalimia kisha mume ugome kumruhusu, ni ngumu na hiyo hutokea tuu endapo mnakuwa hamna mahusiano mazuri na wakwe zako.

Pia kikawaida kama wazazi wameomba inabidi muende wote, kama mna nafasi. Kama haipo basi anaweza kwenda peke yake.

Na kama wakwe zako watakuwa na busara basi wataongea na mume direct, mume ndiye watampa taarifa kisha yeye ndiyo atamjulisha mkewe.​
 
Na kama kuna mahusiano mazuri ataombwa mumewe baada ya kusalimiana,kwanza hatabagua kwa kuwaomba wote wamtembelee.Kama mwanaume yuko bize atamruhusu mke wake aende peke na samahani nyingi kwa mkwe.
 
Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa.

Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​
KASHAOLEWA YUPO CHINI YA UANGALIZI MWINGINE NA MAMLAKA MENGINE (KAMA AMBAVYO ULIKUBALI KUMUOZESHA)

HAWEZI KUTOKA KIENYEJI ENYEJI TU MKUU, LAZIMA AOMBE RUHUSA KWA MUMEWE

Wewe hapo ulipo naamini wife wako hawezi akajitokea tu bila ruhusa na bila kutoa taarifa..akifanya hivyo tunaita ni dharau na kutomtii mume
 
Swala la ww kumlea na kumsomesha ni jukumu lako kama mzazi na swala la yeye kuomba ruhusa Kwa mumewe n Sawa kabisa sababu mwanaume ndie anayemuongoza huyo mwanamke mara baada ya kuwa kaolewa means hayupo Chini yako tena kama mzazi though utaendelea kuwa mzazi wake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom