Hii kiswahili ya kenya na kongo ee bwana

Shirika moja nchini Kenya limeandaa shughuli ya kutaka kuvuja rekodi ya Guinness ya watu wengi kuosha mikono kwa wakati mmoja. kuangalia video bonyeza hapa BBC Swahili - Medianuai - Rekodi ya kunawa mikono

Mlipuko Somalia angalia Video bonyeza hapa BBC Swahili - Medianuai - Mlipuko Somalia


Yanayowasibu wahamiaji weusi Libya

Kwa miaka mingi, jangwa la Agadez, kaskazini mwa Niger, limekuwa kituo cha mwisho kwa wahamiaji kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara, wanaokwenda kutafuta ndoto ya maisha mazuri nchini Libya, au hata Ulaya. Lakini wengi wanaopita katika eneo hilo kwa sasa wanarejea makwao, wakikimbia mapigano nchini Libya, na hasa mashambulio yanayoelekezwa dhidi ya Waafrika weusi, wanaodhaniwa kuwa ni mamluki wanaomsaidia Gaddafi. Salim Kikeke wa BBC anaarifu katika taarifa hii:


bonyeza hapa kuiona video yake BBC Swahili - Habari - Yanayowasibu wahamiaji weusi Libya
 
Maandamano ya bei ya chakula Kenya

Wanachama wa mashirika ya kijamii na baadhi ya raia wameandamana katika miji mbali mbali nchini Kenya kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha.

Kwa sehemu kubwa maandamano yalikuwa ya amani huku waandamanaji wakitoa ujumbe wao kwa mabango wakieleza matatizo yanayowakumba. Maandamano yameitishwa baada ya bei ya mafuta kupanda wiki iliopita na kusababisha bei za bidhaa nyingi kuwa juu.

Kulingana na utafiti wa benki ya dunia bei za vyakula na bidhaa muhimu zimepanda kwa zaidi ya asilimia ishirini kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita.
Mwandishi wetu wa Nairobi Wazir Khamsin alikuwepo kwenye maandamano hayo. Video angalia hapa bonyeza
BBC Swahili - Habari - Maandamano ya bei ya chakula Kenya


Upinzani watawanywa kwa maji ya pinki

Polisi nchini Uganda wamewamwagia viongozi wa upinzani maji ya ragi ya pinki kuwazuia kufanya mkutano wa hadhara uliopigwa marufuku.
Baada ya kuwangiwa maji hayo, kiongozi wa chama cha DP, Nobert Mao alikamatwa.
Wiki hii, vyama vya upinzani vimeongeza kasi yao ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha, hali ambayo imesababisha mapambano kati ya polisi na waandamanaji.
Wakati huoho, Rais Yoweri Museveni amesema ili kupambana na ghasia anataka ianzishwe sheria mpya ya kuwanyima dhamana kwa miezi sita watu wanaokamatwa wakiandamana. Kuangalia video bonyeza hapa BBC Swahili - Habari - Upinzani watawanywa kwa maji ya pinki


 
vua kubwa yaleta taharuki Dar Es Salaam




111222181813_tanzania_flood0_624x351_jamiiforums_nocredit.jpg

111222181813_tanzania_flood0_624x351_jamiiforums_nocredit.jpg



previous
next


Picha 1 kati ya 4


Gari la zimamoto nalo lilikwama kwenye mafuriko hayo mjini Dar es Salaam

Tanzania imethibitisha kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki dunia kufuatia mvua iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo.
Mvua hizo zimeathiri maeneo mengi ya mji wa Dar es salaam. Wengi bado hawajulikani walipo.
Mvua hizi inasemekana ndio kubwa kuwahi kunyesha katika kipindi cha miaka 57.
Picha hizi zimepigwa na Jamiiforums

Chanzo.
BBC Swahili - Habari - Mvua kubwa yaleta taharuki Dar Es Salaam
 
Back
Top Bottom