Hii kazi kiboko....

Hii kazi kiboko....

Habari za mchana .

Almost imepita wiki tangu nilipoleta uzi wangu wenye kichwa cha habari "nahitaji kupumzika ". Nilielezea ni jinsi gani nilikorofishana na mwanaume wangu mpaka ikafikia hatua ya mimi kuacha kazi nikiwa na mpango wa kurudi nyumbani.

Matarajio yangu yakawa sivyo Kwani jamaa aliniwahi na kuniibia pesa yote kisha kutimua. Nikawa sina namna ingawaje kuna mpango wa kazi nilikuwa nausubiri sehemu ila mpaka sasa bado unasua.
Baada ya kukaa kwa siku kadhaa bila mpango wowote ilhali hata kile kidogo nilichobakiwa nacho kinazidi kupungua ,ndipo sasa juzi nikaamua kwenda kutafuta kibarua maeneo ya jogoo huko mbezi(chemicotex).. E bwana ee si mchezo nilipiga kazi mpaka nakuja kutoka sitamani hata kutembea,, mwili wote unauma kama sio wangu.. Jana nimepiga moyo konde nimeenda natumaini Mungu atanisaidia na soon nitapata ajira kulingana na proffessional yangu..
..Tangu jana yule muhuni ananipigia simu lakini nikifikiria jinsi ninavyoteseka kwa sababu yake,,sipokei...... Let it go!
Mwil umechoka sitamani ata kutembea.." ulipiga kazi gan mkuu bado sijaelewa....!
 
hapo sasa yakupasa utumie maujanja yako...fanya kama vile unamkubali huyo bwana kisha mpige kizinga cha kufa mtu....
 
Back
Top Bottom