naweza kutabiri anguko kubwa sana la utawala huu,
nchi imepoteza rslimali nyingi ku~decentralise,anakuja mmoja ana centralise system ya utawala.
Ninachokiona,maamuzi mengi sana katika halmashauri yatachelewa kwa kuwa utabidi wakuu wa mikoa/wilaya/ wakurugenzi nchi nzima wawasiliane na ikulu kwanza.
Maamuzi yakichelewa haimaanishi muda utasimama,2020 iko palepale.
Sasa hivi halmashauri zitaacha kupima viwanja kwa woga wa kuchukua maeneo ya wananchi hata kama wana hela ya kuwafidia,
sasa hivi watu watajikusanya kikundi,watavamia shamba la mtu,watalima,hata kama muhusika ana nyaraka zote za umiliki,zitafutwa,wananchi wanafundishwa kutofata taratibu na sheria.
uhuru wa serikali za mitaa umepotea,uhuru wa kimaamuzi ya wakuu wa wilaya na watendaji umekwisha(sasa huwezi hata kusikia ATCL imekaa na bodi yake kujadili ununuzi wa ndege,ananunua mtu mmoja tu)
Bora hata maamuzi yangekuwa centralised kiserikali huko serikali kuu kwa maana mawaziri,wakuu wa mikoa,watendaji wa taasisi,sasa maamuzi yako kwa MTU mmoja!!
TRA wakiamua,yeye anatengua maamuzi,nini maana ya kuipa uhuru kimaamuzi TRA?
Huyu mtu mmoja ana utaalam wa kila jambo ?jack of all trades?!