Kisasi kizuri ni mafanikio. Mh Magufuli kaza buti Mh Makonda kaza buti. Mafanikio yenu si ya kutafutwa kwa tochi kila mwenye milango ya fahamu hata mmoja atafahamu mafanikio yenu. Kuimarika shirika la ndege, mateja kupungua na wauzaji kukamatwa, foleni Dar kwisha na tija kuongezeka, reli ya kiwango, viwanda vya sukari ya kukidhi mahitaji yetu,watumishi wenye kuwajibika na kuto huduma bora kwa wananchi, serikali kuhamia Dodoma na kusogeza huduma za kiutawala kwa wananchi. Hivi ndivyo vitakuwa vigezo vya kuipima kama serikali inaweza kuwaletea watu wake maendeleo.