Hii katuni ya Kikwete vipi?

JK anatuaibisha sana, hana mashiko. jamaa hailewi wala hasikii. inawezekana hana nyumba nzuri bongo au bado ikulu inakarabatiwa nn?
 
Inanikumbusha ule wimbo wa zamani aka zilipendwa "...Bwana nipe pesa, watoto wana njaa....majirani wanasema fungeni milango anakuja..." Analitia taifa aibu!
 
nadhani mheshimiwa akistaafu katika vitu atakavyovimisi sana ni safari.

Kiasi alichokusanya, pensheni atakayolipwa pamoja na fungu la matunzo atakalokuwa analipwa linatosha mno kwa yeye kuendelea kubembea majuu. Usisahau pia kuwa ana fursa ya kwenda majuu kucheck afya kwa fedha za wavuja jasho labda katiba mpya ifute hayo.
 
2495864_orig.jpg
hii nikubwa kuliko...
 
Anasafiri sana huku akijua hakuna maafisa wa ngazi za juu jeshini mwenye uchungu na nchi yao. Kama jeshi lina maafisa wenye kuipenda nchi yao, basi kikwete anastahili kupinduliwa. Sijui ntapingwa ban?
 
Mbeya kaja Huku Mara mbili tokea awe Rais lakini USA kaenda Mara 15 inaelekea mbeya ni mbali sana kuliko USA!!!!

Mlimpopoa kwa mawe! Anakuja kwa tahadhari. Mbeya hakuna wanunuzi wa Kigamboni. Mbeya hakuna mabenki ya Kiswiss. Mbeya kuna "mbalaga" tu, yeye hajakulia mbalaga(ndizi zilizopikwa).
 
Mh rais kikwete nenda kwa marafiki zetu huko ughaibuni ili upate miradi mbalimbali ya kuendeleza uchumi wa nchi yetu.hakuna nchi inayoweza kuendelea kiuchumi bila kuwa na uhusiano mzuri na nchi marafiki.
 
Nchi zote zilizowekewa vikwazo vya kiuchumi huporomoka uchumi wao.kwa sisi hatuna vikwazo vya namna hiyo kikwete lazima aende pale anapoona kuna maslahi kwa nchi yetu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi
 
Kupiga ruti si issue, issue ni je hizo ruti zinatufaa nini? Labda wengi wetu hatuna taarifa za yatokanayo. Hapo ndiyo unapoona kupwaya kwa kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu. Wanachojitahid ni kutoa taarifa za rambirambi na vitu safari za rais. Kutoa mlishonyuma wa safari hizi, hawafanyi. Huenda hakuna yatokanayo na hiz trip??
 
Back
Top Bottom