Hii kasi ya Nyalandu imetokea wapi?

Hii kasi ya Nyalandu imetokea wapi?

Tangu waziri kagasheki ang'atuke kwenye kiti cha uwaziri, naibu wake ameibuka ghafla na kutaka kujionesha kama ndie mtu mwenye dawa ya ugonjwa sugu wa ujangili katika wizara hiyo. Kwa baadhi yetu, tunaona kama spidi hiyo ni gia ya kufukuzia kiti alichoachia boss wake! Lakini swali la msingi ni je, mnofu uliowashinda watangulizi wake karibia 6 yeye ataweza kuumeza?! TAFAKARI!

Itakuwa imetokea kwa Mtogole.
 
Huyu Lazaro Nyalandu anachofanya sasa hivi ni usanii tu, siku zote alikuwa wapi? Nani alikuwa anamzuia kufanya kazi yake, tumuone eti kacharuka ghafla sasa hivi. Wanasema "life is not a dress rehearsal," ila Lazaro anafanya role rehearsal ili watu wasiokuwa na fikra sahihi wamuone ni mchapa kazi na apewe cheo cha Waziri wa Maliasili na Utalii kuchukua nafasi ya Khamis Kagasheki. Huyu Lazaro naye ni mzigo tu, siku zote alikuwa wapi asichukue hizo hatua. Kazi kuzunguka na media tu kila kona ili aonekani ni waziri jembe.

Kwenye Operesheni Tokomeza naye amehusika, kwani alikuwa ni naibu waziri wa wizara na accountability ni lazima viongozi wote wakuu wa wizara wachukue, siyo waziri tu. Kwa heshima ya roho za wananchi zilizopotea kwenye Operesheni Tokomeza, ni lazima viongozi wafuatao wa wizara ya maliasili na utalii nao watolewe waletwe viongozi wapya:

1. Naibu waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu.
2. Katibu Mkuu
3. Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama Pori
4. Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA
 
Nyalandu is doing his duty.Wala tusishangae asingefanya hivyo wote tungemuona kenge.Kagasheki alikuwa incharge hivo nyalandu asingeweza mfunika bosi wake.Kumbuka mwakyembe alipokuwa na Magufuli. Nyalandu ana jitahidi hata kama anatafuta uwaziri shida iko wapi?Strategy yake ameanza kudeal na wafanyakazi nadhani ni step nzuri...next aende kwa ma papa.
 
Watanzania bwana!! Mtu afanye kazi, kosa; akiwa hashughuliki, ataambiwa mzigo! Heri walioamua kutokuwa wanasiasa!

acha kumtetea maana hata yeye alitakiwa kuondoka maana na yeye ni mmojawapo wa wizara husika. Swali je! Alichukua hatua gani kwa muda wote alioteuliwa hadi hii leo?
 
Amechoka kuwa waziri mdogo anataka awe waziri mwenye dhamana.
 
nyalandu anatabia kuwa na kasi fulani hivi unakumbuka alipokuwa naibu biashara na viwanda alipiga mzigo mpaka cyril chami akaonekana naibu wakati ndio alikuwa waziri....
 
Madaraka kwa njia ya majungu, huyu jamaa ni bingwa wa kuyapika
 
Tangu waziri kagasheki ang'atuke kwenye kiti cha uwaziri, naibu wake ameibuka ghafla na kutaka kujionesha kama ndie mtu mwenye dawa ya ugonjwa sugu wa ujangili katika wizara hiyo. Kwa baadhi yetu, tunaona kama spidi hiyo ni gia ya kufukuzia kiti alichoachia boss wake! Lakini swali la msingi ni je, mnofu uliowashinda watangulizi wake karibia 6 yeye ataweza kuumeza?! TAFAKARI!

Kuna uzi uliwekwa hapa siku chache zilizopita ukisema jamaa aliwaweka mahali waandishi akawapa mvinyo na bahasha ili wampambe kwenye media zao, mkulu amuone anafaa kuvaa biatu vya Kagasheki, ukiunganisha mistari inakupa nini hapo???? Nchi ya kitu kidogo.
 
Yaani watanzania sijui uwafanyie nini, ukifanya vizuri, nguvu zimetoka wapi, ukizembea wewe ni mzigo wa Nape na Dentist. kuwa wavumilivu hiki ni kipindi kigumu.
 
Tangu waziri kagasheki ang'atuke kwenye kiti cha uwaziri, naibu wake ameibuka ghafla na kutaka kujionesha kama ndie mtu mwenye dawa ya ugonjwa sugu wa ujangili katika wizara hiyo. Kwa baadhi yetu, tunaona kama spidi hiyo ni gia ya kufukuzia kiti alichoachia boss wake! Lakini swali la msingi ni je, mnofu uliowashinda watangulizi wake karibia 6 yeye ataweza kuumeza?! TAFAKARI!

Kwa hiyo ulitaka shughuli za Wizarazisimame mpaka tupate waziri mwingine? Mbona tumekuwa watu wa longolongo nyingi nchi hii?
 
Tangu waziri kagasheki ang'atuke kwenye kiti cha uwaziri, naibu wake ameibuka ghafla na kutaka kujionesha kama ndie mtu mwenye dawa ya ugonjwa sugu wa ujangili katika wizara hiyo. Kwa baadhi yetu, tunaona kama spidi hiyo ni gia ya kufukuzia kiti alichoachia boss wake! Lakini swali la msingi ni je, mnofu uliowashinda watangulizi wake karibia 6 yeye ataweza kuumeza?! TAFAKARI!

Mfumo wa Serikali ya JMT ni mbovu...Unamfanya Naibu Waziri kufuata Maelekezo ya Boss wake ambaye ni Waziri..hivyo, hawezi kuwika chini ya Utaratibu huo...Tumpe muda, labda aweza. Na pengine anaitaka nafasi ya Kagasheki....atashangaa!
Hata Mwakyembe Chini ya Magufuri alikuwa ni just a civil servant...
 
Yani mtu akifanya Kazi kosa, akifanya shughuri shida! akishughulika ndo hamtaki.

Alikuwa wapi asifanye kwa kasi aliyonayo sasa? Alitakiwa ampe ushirikiano Kagasheki hakufanya hivyo sasa ndo anakuja na mbwembwe! Hana lolote huyo zaidi ya kusaka uwaziri kamili! Halafu huyu jamaa alikuwa viwanda na biashara, Chami katimuluwa yeye kabakia! sasa Kagasheki naye yamemkuta kabakia yeye! Inaelekea bibi yake mzaa baba yake wa mama mkubwa na mdogo pado wapi pale Singapori!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom