Hii kasi ya kununua madawati ni ya dhati au unafiki?

kinguo

JF-Expert Member
May 27, 2016
440
318
Habari wanajukwaa.Nadhani mko pouwa mkiendelea na majukumu wengine wakiwa kwenye vilinge wakipata moja moto moja baridi na story za hapa na pale.

Naomba niende kwenye mada. Hivi hii kasi ninayoiona kuhusu ununuzi wa madawati ni kweli hawa viongozi wanamaanisha au ni unafiki fulani tu unaendelea. Nauliza hivi kwa sababu moja tu. Wote tunajua hamna serikali mpya ambayo iko madarakani ni hawahawa ndio walikuwepo toka huko nyuma.

Na sio kwamba labda sasa hivi ndio tunavuna miti ya mbao sana tofauti na huko tulikotoka. Nini hasa maana kama ni mateso.watanzania wameyapata miaka nenda rudi. Kwahiyo hoja yangu ni kweli wanatenda kwa kuumizwa na umasikini wetu au ni unafiki tu ndio umetamalaki.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni unafiki 100%

Hata hivyo mimi nasema acha wamalize madawati na baadaye warudi kuchapa mijeledi wananchi kuchangia ukamilishaji wa magofu ya vyumba vya maabara ktk kila shule ya sekondari ya kata na zahanati kwa kila kijijiji!!

Baada ya hapo tunanaanza kuchangishana visenti kwa ajili ya kuanza kuianzisha " Tanzania ya viwanda vya Magufuli!!"

Hapo sasa ndo patamu balaa maana ni matrilion ya shilingi yanahitajika na wakati huo kitakuwa ni kipandi cha karibu karibu na uchaguzi mkuu wa 2020!!
 
Back
Top Bottom