Hii 'kamata kamata' maana yake nini?

Hii 'kamata kamata' maana yake nini?

Nabado muda wakucheka na nyani umeisha

Watu walifanya watakavyo kana kwamba hakuna serikali.

Police fanyeni kazi kwa usalama wa Watanzania
 
Katika hali ambayo haieleweki lengo lake ni nini,kumetokea kamatakamata ya wapinzani jijini Mbeya.

Juzi usiku aliyekuwa mwenyekiti wa BAVICHA Mbeya mjini aliandika kwenye group la chama Mbeya kuhusu oparesheni UKUTA. Jana jioni amekamatwa na hajulikani yupo Kituo gani hapa Mbeya japo taarifa zinadokezwa kuwa atasafirishwa kupelekwa Dar, juzi pia aliyekuwa katibu wa Moses naye amekamatwa.

Kuna kina mama walokomenti kuhusu operasheni UKUTA taarifa zilizopo wanatafutwa na polisi na wanaishi kwa kujificha mpaka saa hii, na cha ajabu zaidi simu ya Moses haipatikani ila WhatsApp anaonekana kuwa online.

Hivi hii kamatakamata ni kwa maslahi ya nani,nani anawatuma polisi?? Rais anajua kweli kinachoendelea kwa wananchi wake au polisi wanajiamulia tu?
Polisi mnapokamata watu hovyo namna hii mnajua mnachojenga mioyoni mwa ndugu,jamaa na rafiki zao?

Jamani tusifikishane huko, nchi haiwezi endelea kwa kuwekeana visa. Kama lengo letu ni kujenga nchi lazima tukemee huu uonezi, haiwezekani watu wazibwe midomo kwa njia za kikatili. Binadamu huchoka, tuchague kufuta vyama vingi au tuache watu wafanye siasa, tuache watu waongee.

Msije sema hatukuwahi onya haya mambo
bro maisha yamekuwa kama tuko GAZA; vijana wa pikipiki nao ahadi walizopewa zimeyayuka, kila uchao kuna gari lenye namba za kiraia, Toyota Z 322 AN, kiongozi wa msafara ni afande MWITA, anaongozana na kundi la vijana wamevalia nguo za kiraia, kazi yao ni kutafuta hela tu kupitia vijana wa bodaboda . ukiwapa hela wanakuachia , ukiwa huna wanakupeleka mahakama ya jiji, vijana wametumika wakati wa uchaguzi , sasa hivi thamani yao haiko wanaonekana wanachafua jiji sijui huko tuendako hali itakuwaje.
 
Ngoja tuone hiyo kazi ya mapolisi yenu itakapoishia,itakula kote
 
bro maisha yamekuwa kama tuko GAZA; vijana wa pikipiki nao ahadi walizopewa zimeyayuka, kila uchao kuna gari lenye namba za kiraia, Toyota Z 322 AN, kiongozi wa msafara ni afande MWITA, anaongozana na kundi la vijana wamevalia nguo za kiraia, kazi yao ni kutafuta hela tu kupitia vijana wa bodaboda . ukiwapa hela wanakuachia , ukiwa huna wanakupeleka mahakama ya jiji, vijana wametumika wakati wa uchaguzi , sasa hivi thamani yao haiko wanaonekana wanachafua jiji sijui huko tuendako hali itakuwaje.
Mungu pekee ndo unajua tuendako
 
Mimi nashauri wangefuta vyama vingi,waache tutafute mamlaka kwa kupinduana maana hamna tija ya vyama vingi wakati vinabinywa.
 
Katika hali ambayo haieleweki lengo lake ni nini,kumetokea kamatakamata ya wapinzani jijini Mbeya.

Juzi usiku aliyekuwa mwenyekiti wa BAVICHA Mbeya mjini aliandika kwenye group la chama Mbeya kuhusu oparesheni UKUTA. Jana jioni amekamatwa na hajulikani yupo Kituo gani hapa Mbeya japo taarifa zinadokezwa kuwa atasafirishwa kupelekwa Dar, juzi pia aliyekuwa katibu wa Moses naye amekamatwa.

Kuna kina mama walokomenti kuhusu operasheni UKUTA taarifa zilizopo wanatafutwa na polisi na wanaishi kwa kujificha mpaka saa hii, na cha ajabu zaidi simu ya Moses haipatikani ila WhatsApp anaonekana kuwa online.

Hivi hii kamatakamata ni kwa maslahi ya nani,nani anawatuma polisi?? Rais anajua kweli kinachoendelea kwa wananchi wake au polisi wanajiamulia tu?
Polisi mnapokamata watu hovyo namna hii mnajua mnachojenga mioyoni mwa ndugu,jamaa na rafiki zao?

Jamani tusifikishane huko, nchi haiwezi endelea kwa kuwekeana visa. Kama lengo letu ni kujenga nchi lazima tukemee huu uonezi, haiwezekani watu wazibwe midomo kwa njia za kikatili. Binadamu huchoka, tuchague kufuta vyama vingi au tuache watu wafanye siasa, tuache watu waongee.

Msije sema hatukuwahi onya haya mambo

Usitafute kiki za kiki, eti whatsapp yupo ila hapatikani nendeni polisi mtoe taarifa, kaka yupo huko mtamkuta, kwa nini afichwe sisimizi tu huyo. Kama amefanya kosa basi si ajabu kushikiliwa, hata wewe na mimi tukifanya kosa tutashikiliwa bila kujali Chadema au huna chama. Tua Ngoma
 
Busara itumike kwenye mazingira tuliyonayo sasa. Ukweli ni kwamba vyama vya siasa vinaendelea kuimarika huku vikinyang'anyana wanachama na kuwavutia wananchi kwa kila anayeona ni chama gani kinamfaa. Hili halikwepeki na ni ngumu sana kulifuta. Huo ndo mchango wangu
 
Usitafute kiki za kiki, eti whatsapp yupo ila hapatikani nendeni polisi mtoe taarifa, kaka yupo huko mtamkuta, kwa nini afichwe sisimizi tu huyo. Kama amefanya kosa basi si ajabu kushikiliwa, hata wewe na mimi tukifanya kosa tutashikiliwa bila kujali Chadema au huna chama. Tua Ngoma
Wewe kibaraka wa njaa sikiliza,kiongozi amekamatwa na simu yake,simu akipigiwa haipatikani na online yupo WhatsApp, tutafute kiki ya nini wakati watanzania wenye akili timamu laki saba walitupigia kura kutupeleka ikulu,kiki anatafuta aliyepata kura za mboga,akaiba nyingine ili awe kiongozi wa tusiomchagua
 
Mku akipotea taarifa hupelekwa na polisi, mmepeleka?
 
Back
Top Bottom