Hii kali

Laiser

Member
May 19, 2011
15
6
Mume karudi nyumbani akiwa njwii, maji yamemfika mpaka shingoni. Mke akamwuliza, Mume wangu mbona umelewa hivi, twende nionyeshe ulikuwa unakunywa wapi. Mume akampeleka kwenye baa ya mama muuza gongo. Mama muuza gongo akasema kweli mume wake alikuwa hapo akipata kilaji. Mke kwa hasira akamwambia mumewe, siku amabayo utatia miguu yako hapa nitakuacha. Mume akaomba msamaha kuwa hatatia miguu hapo kwenye baa tena. Kesho yake yule mama muuza baa alimwona yule Baba akiigia baa kwa mikono na miguu juu, akamuuliza kulikoni? mzee wa watu akajibu, wewe umesahau kuwa jana nilimwahidi mke wangu kuwa sitatia miguu hapa, sasa nimekuja kwa mikono mwenzio sitaki kuachika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom