Hii kali, nimeikuta Guest House

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,696
Usiku wa kuamkia leo nikiwa ktk mihangaiko yangu ya biashara Bunda mjini nilichukua chumba ktk nyumba moja ya kulala wageni, wakati nikijisajili ktk daftari la wageni nikawa nimekutana na mteja aliyekuwa kaandika jina lake na details zake ktk namna ya ajabu Sana, cha ajabu nilibaini kuwa, wahudumu hawa huwa wazembe Sana kusoma walichoandika wateja.
Ilikuwa hivi :
Jina la mteja :Tunaonewa Jamani.
Mahali Unapotoka :Sijui.
Mahali Unapokwenda :ili iweje?
Passports number :666.
Sehemu Uliyozaliwa :muulize mama.
Kazi yako :Mzurulaji.
Uraia Wako :Kuzimu.
Chumba namba :000.000.


Wakuu, sina utani na nyie, jamaa alikuwa kaandika Kwa mwandiko wa mcharango Sana, lakini unaosomeka, na niliposoma na Kumwita muhudumu ili aone, akadai hata yeye hajui kuhusu habari za huyo mteja.
Nilipotaka kupiga picha maandishi hayo akanikatalia kabisa yule muhudumu akidai nitawaharibia biashara, wakuu hii imekaaje?
 
Lala humo uje uibukie kuzimu,mtu na akili zake hawezi kufanya hayo,jini hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom