Hii issue inanikosesha raha....naomba maoni yako

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Posted by queenkami | May 15, 2012

Hello wapendwa wangu.

Kuna ndugu yangu wa damu alinifanyia jambo ambalo kawaida ndugu hawezi kumfanyia ndugu yake,ni kitendo cha laana,abomination,kwa jinsi nilivyo sikujua kamwe kama naweza ku expirience kitu kama hichi,siku zote nilizani hufanywa na watu kutoka kwenye koo zenye laana.

Nilikuja kujua siri hii baada ya ndugu yangu huyo kugombana na rafiki yake ambaye ndiye aliyeitoa siri,niliugua depression,nilifikia hadi kufikria kujiua,maisha yangu yote nikayaona hayana thamani,nilikua najisikia vbaya sana.

Hata hivyo nilifikia sana na kwa vile mim nimeokoka nikaona kwa vile kilichotokea kimeshatokea nikachagua kumsamehe ndugu yangu,nikaona siko tayari kumpoteza ndugu yangu japo nilijua ana roho ya ajabu.

Hii siri sikumweleza mtu yeyote bali nilimweleza mama yangu tu ili ajue mambo ambayo mwanae nimefanyiwa.

Basi yule ndugu yangu aliposikia kuwa nimemueleza mama akanipigia kuwa kuanzia dakika hiyo tunayoongea nijue kuwa siko katika list ya ndugu zake,hanijui nisimjue.Pmaoja ya kwamba mim ndiye niliyetendwa nikambembeleza huku nikilia kuwa sisi ni ndugu tusiruhusu kitu chochote kitutenganishe.

Katika simu hiyo sikutaka kuongea kwa hasira wala kwa kugombana bali yeye ndo aliyekua yuko juu as if mim ndiye mkosaji,akisisitiza kuwa nisimjue.

Sikutaka aniombe msamaha wala nini nilitaka tu maelewano,tuwe tu kama jinsi ambavyo ndugu wanatakiwa kuwa lakini jinsi nilivyojishusha alichukulia sijui kama mim najiona ndiye mkosaji au vipi na ndivyo alivyozidi kunionesha chuki na kujitahidi kuongea uongo watu wanione mim ndiye mbaya na katu hakulegeza moyo wake.

Nikikutana naye mjini huwa nasimama kwa lengo lakusalimiana naye ila yeye ananipita kama vile ni invisible sionekani,wakati mwingine nampigia simu anavyonijibu naishia kujisikia vibaya.

Sasa ikafikia wakati niasema kutendwa nitendwe mim kujimbembelezesha nijibembelezeshe mim,nikasema kama noma na iwe noma nimechoka,na mim nikaamua kukaa kimya.

Kinachoniumiza ni kwamba,anawaambia watu eti mim najifanya mlokole lakini siongei na ndugu yangu wa damu.
Pili kwa vile yeye ndiye mkubwa watu wananilazimisha nimuombe yeye msamaha eti ili tu yaishe lakini naona nikimuomba msamaha itakua wa unafiki sababu ndani ya moyo wangu najua sijamkosea.

Wakubwa wa hapa naombeni mniambie nyie mngefanyaje hapa.

Shukrani
 
Last edited by a moderator:
Point umeicamouflage. Hapa ni JF speak out your mind. Taja chanzo cha kuchukiana. Je alijaribu kuacha stedi upotee for keeps au alijaribu kutoa kafara?
 
Hauko tofauti sana na Hajjat aliyenasa SMS za mapenzi ktk simu ya bwana wake, akaishia kubembeleza mme wake! Mtu anafanya makosa then unabembeleza! Nonsense.
 
Ndugu yangu,
Umesema ya kuwa umeokoka katika maelezo yako, ukisoma Efeso 6 anaongea juu ya vita vyetu si juu ya damu na nyama. Vita vyoyote kabla havijawa dhahiri katika ulimwengu wa mwili vinaanza kwenye ulimwengu wa Roho.

Nasi kwa watu tuliookoka tunaupendeleo wa kujua nini kinakuja hata kabla hakijatokea na au ikitokea kabla ya kujua ni vizuri kumshirikisha Mungu katika maombi ili kujua kama maneno uliyoambiwa ni ya kweli au ni mpango wa adui. Kama ni kweli au uongo basi Mungu akuonyeshe njia ya kutoka na kuendelea mbele na hili litakuwa ni suluhisho la kudumu.

Inawezekana kabisa nduguyo kasema au kafanya jambo ovu, kumbuka shetani anaweza kutumia mtu yeyote akuharibu wala si kitu cha ajabu. Ni wakati wa kuomba kwa bidii na kuutafuta uso wa Bwana na tena ukitanguliza msamaha (Mathayo 6:12). Usiruhusu kitu chochote kiondoe amani yako, mwangalie Yesu Kristo ndiye Bwana wa amani (2The 3:16).
 
sitaweza kutoa ushauri wangu bila wewe kufunguka kilichokusibu.. Hata sasa tumeshapata maswaibu mazito ya kumwambia mama pekee lakini kwa sasa tunafunguka ukweli tunatua mzigo..
 
huwezi kuomba ushauri at the same time unamficha mambo unayoombea ushauri.....kama uko serious unataka ushauri sema ukweli...i mean every thing in and out...ukificha tu ujue unaathiri ushauri utakapewa.
 
huwezi kuomba ushauri at
the same time unamficha mambo unayoombea ushauri.....kama uko serious
unataka ushauri sema ukweli...i mean every thing in and out...ukificha
tu ujue unaathiri ushauri utakapewa.

kajificha kwenye ID. anaficha na details za tatizo!
 
sasa tutakusaidiaje dada yetu mpendwa maana tatizo hatulijui kama vipi mweleze mama ambaye tatizo analijua atakusaidia kwa ushauri japo tungeshiliki wote ingekuwa nzuri zaidi
 
Pointless. Sijaelewa kitu, vipi tukusaidie wakati huko muwazi. Bado hujawa tayari kupata msaada.
 
kweli. weka mambo hadharani tukusaidie!

sitaweza kutoa ushauri wangu bila wewe kufunguka kilichokusibu.. Hata sasa tumeshapata maswaibu mazito ya kumwambia mama pekee lakini kwa sasa tunafunguka ukweli tunatua mzigo..

huwezi kuomba ushauri at the same time unamficha mambo unayoombea ushauri.....kama uko serious unataka ushauri sema ukweli...i mean every thing in and out...ukificha tu ujue unaathiri ushauri utakapewa.

kajificha kwenye ID. anaficha na details za tatizo!

sasa tutakusaidiaje dada yetu mpendwa maana tatizo hatulijui kama vipi mweleze mama ambaye tatizo analijua atakusaidia kwa ushauri japo tungeshiliki wote ingekuwa nzuri zaidi

funguka ushauriwe c unajua mficha uchi hazai

Pointless. Sijaelewa kitu, vipi tukusaidie wakati huko muwazi. Bado hujawa tayari kupata msaada.

Mtanisamehe bure ndugu zangu kufunguka zaidi ya hapo is a big HAIWEZEKAZI.
Kuna coments nilishauriwa mwanzo naona zimepotea,mbona hao wenzenu waliweza kunishauri kwa maelezo haya haya niliyotoa.
Sasa kwa mfano nikisema alitaka kuniwekea sumu,au kunitoa kafaraka,au alisababisha nikabakwa au alinibaka,au alinithurumu au alinifanyaje sijui kitu ni kile kile tu kutendwa,nimesema kanitenda kitu ambacho ni kikubwa.
Anyway nawashukuruni kwa nia ya kutaka kunisaidia.
Kufunguka sitafunguka hapa mtanisamehe bure.
Wale wapendwa wangu woote mlionishauri kwenye coments za mwanzo zikapotea nawashukuru sana na pia ushauri ule mlionipa ndio nitaufuata.
Sijui kama nitawakumbuka nyote mlionishauri mwanzo kwenye coments zilizopotea ila asante sana Kongosho namkumbuka yatima lol Lizzy@Mr Rocky,@Smille BADILI TABIA madame X na gfsonwin vile vifungu vya biblia vimetia amani na faraja.Pia nitakuPM unipe yale madesa uliyoongelea.
 
Last edited by a moderator:
Hauko tofauti sana na Hajjat aliyenasa SMS za mapenzi ktk simu ya bwana wake, akaishia kubembeleza mme wake! Mtu anafanya makosa then unabembeleza! Nonsense.

Mtu mwenyewe hajasema alichofanyiwa wewe umekimbilia kutoa hukumu kwa ushahidi upi?
 
siraha ya ushindi ni maombi! Nainaonekana hujui wajbu wako km kweli umeokoka, unambembeleza adui! Poor queen
 
Sa' unataka kushauliwa kuhusu nini?, watu wengine bana, unapoteza muda wako kuandika passwords, halafu unakuja hapa kuomba ushauri. Eleza kwa uwazi nini kilichosababisha wewe na huyo ndugu yako mkatofautiana ndo kisha uombe huo ushauri unaotaka kupewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom