Hii ishu imekaaje tanapa, wadau msaada tafadhali

Hii ishu imekaaje tanapa, wadau msaada tafadhali

Eistein

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
1,107
Reaction score
482
habari zenu wadau
naomba kwa anayeweza kusaidia kufahamu ukweli juu ya hili tukio, nadhani kuna wengine humu yameshawakuta

1. Kuna mdau mmoja amenistua kuwa kuna jamaa anasema anafanya kazi tanapa anatumia simu ya 0716473432, anawapigia simu watu mbalimbali kuwaambia kuna nafasi waliapply hapo tanapa miezi kama 5 hivi imepita so huyo bwana anasema kuna nafasi saba anaweza saidia kupata hizo dili na jumatatu 28/10/2013 anawaambia hao watu waende arusha tanapa hq, lakini wanapaswa kutoa rushwa ya laki 5, lakini kwa kuanzia kabla ya kwenda unapaswa kumtumia laki 1.

Fikiria akiwapata watu 5 tu kwa siku tayari jamaa ana laki 5....

Nimejaribu kumpigia simu huyu bwana anayesema anafanya kazi tanapa tangu jana hapokei simu . Nimefanya uchunguzi wangu binafsininaonyesha huyu mtu hayupo tanapa.

Wadau haya mambo nahisi niutapeli, lakini inakuwaje system inaruhusu mambo haya.. Nadhani ni hatari kwa image ya mashirika mbalimbali.. Maana inaonekana kuna vitendo vya rushwa maeneo ya tanapa



sasa wadau nimelileta hapa , kama angalizo kwa wengine wasije kulizwa, lakini pia kwa wadau wa tanapa kutoa hari halisi ikoje kuhusu hizi taarifa.

Maana navyojua tanapa hutangaza hizi kazi aiza wenyewe au kupitia recruting agency....

Wadau tukae chonjo ukosefu wa ajira unasabisha utapeli wakila aina sasa. Hata kama tunatafuta kipato ndugu zangu lakini si kwa mtindo huu...

Tafakari chukua hatua.
 
atakayetuma naye atakuwa amevurugwa\

MKUU WATU WAMESHALIZWA SANA HIZO ISHU WENGINE KWENYE MIKOPO YA VIKAMPUNI UCHWARA, NA HUKU KWENYE AJIRA NDIO USISEME UMESAHAU MWAKA JANA KUNA MKE WA KIGOGO MMOJA WA POLISI ALIKUWA ANAPOKEA FEDHA KAMA HIZO ETI AWAFANYIE MPANGO WATU WAINGIE USALAMA WA TAIFA, UMESAHAU YA DECI??

UKOSEFU WA AJIRA NA WIMBI LA VIJANA KUWA WENGI NI BOMU LINALOKARIBIA KULIPUKA NA HIZI NDIO DALILI ZAKE
 
Back
Top Bottom