Hii iPhone siielewi

Martine Tibe

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
221
156
Juzi nilinunua simu aina ya iPhone NJ, nilipoiwekea simu card ikaandika emergence call. Nikabadili SIM card tena ikaandika emergence call, na chaji ilikuwa imekaribia kuisha, ilikuwa na 1% ambapo baadae ikazima kabisa.

Nikaamua kuichaji, nilipoichaji kwa muda ilionyesha inapeleka lakini nilipoiwasha haikuwaka kabisa na sasa haipeleki chaji hata kidogo na ukiishika kwa pembeni kuna kama shoti.

Je nifanyeje?
 
Mmmhh kama ingekuwa imeandika "emergence call " ningeweza kukusaidia.

Alafu ni iPhone gani? Maana ya kwangu ilikuwa ikizima nikiweka kwenye chaji inawaka yenyewe.
 
Martine Tibe,
Mkuu kununua simu used isiyo na guarantee ni aina ya uchomaji wa moto wa fedha zako.

Maana yake ni kwamba, huko zinakotoka, kuna matatu; aidha mmiliki aliiharibu na inamsumbua akaamua kuidump sokoni, iliporwa kwa mtu bila kutenguliwa password ama mmiliki ni muenda na wakati, kila toleo anataka alitumie, likitoka jipya anauza lililopita.

Sasa inategemeana simu hiyo ilitokea kwenye mikono gani.

Vinginevyo mkuu rudi kwenye duka ama kijiwe ulikoinunulia wakubadilishie nyingine.

Haiwezekani mke umemuoa jana tu hajawahi ha 'kukupikia' mara moja, anaanza maroroso yake.
 
Mmmhh kama ingekuwa imeandika "emergence call " ningeweza kukusaidia.

Alafu ni iPhone gani? Maana ya kwangu ilikuwa ikizima nikiweka kwenye chaji inawaka yenyewe.
Kama imeandika emergence call ningefanyaje? Maana hata haiwaki kwa sasa na ukiweka chaji ukaishika pemben kuna shoti.

IMG_20191103_094110_3.jpeg
IMG_20191103_094121_5.jpeg
 
Kuna vimaandishi fulani huandikwa designed in California, assembled in China kama sijasahau, huandikwa chini ya neno iPhone. Hapo sivioni? Na nahisi hiyo sio iphone halisi, sijawahi ona iphone nyeusi ina button nyeupe, kwanza iPhone NJ ndo simu gani? Sijawah isikia hiyo version
Kama imeandka emergence call ningefanyaje?.maana hta haiwaki kwa sasa na ukiweka chaji ukaishka pemben kuna shoti.View attachment 1252582View attachment 1252583
 
Vitu vya mnada mara nyingi ni vibovu kamwe usinunue vitu vifuatavyo, smartphone, printer, Music system, TV. hakikisha unanunua kitu amabcho unaweza kukikagua hapo kwa papo bila mahitaji , ooh betri imekufa ukibadili itawaka,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom