Mkuu, inawezekana hujazoea interviews za Organizations ambazo zina international presence duniani, huo ni utaratibu wa kawaida kabisa wa interviews kwa mashirika ambayo international.
Na ni lazima kwa sababu key decision makers unakuta wako nje ya nchi kama hivyo London, Nairobi, Kwa hiyo ni lazima interview iwe virtually kama hizo zoom na zinazofanana na hizo. So, wengine wanakwepo nchini, ila ambao wako nje basi wana-join virtually. Inaonekana bado ni mgeni sana kwenye issues za interviews.
Huo muda wa interview pia ni kawaida kabisa, kwanza mbona ni mchache, usilinganishe na interviews za utumishi za dakika 5. Mimi nilishagonga interview lisaa limoja na nusu.
Kwa hiyo kaa kwa kutulia, endelea kumuomba Mungu uwe umepita upate hiyo kazi... Uzuri wa interview za hivyo hazina figisu, ni kwa merit tuu, kwa hiyo hata ukikosa huwezi ukasema kuwa ulipigwa fitna.
All the best.