Hii interview imenishangaza

Jitahidi uendane na speed/teknolojia ya mwajiri wako mpya kama utapata...

Mana haya mambo ya VTC ni kawaida kwa dunia ya sasa..
 
Wakuu,


Sijui mimi ndiye mshamba wa haya mambo ya interview au vipi!

Kuna kampuni walinipigia niende kwenye interview, siku hiyo nimefika receptionist akanipokea vizuri then akanipeleka boardroom, nikajua kule ntakutana na panelists, cha ajabu nikakuta tu screen kubwa mezani. Then yule panelists akasema kwa kunitaja jina kuwa Joseph is here for interview.

Then nikaona watu wako kwenye screen wananikaribisha kwenye interview, wakajitambulisha kuwa mmoja alikua mmama wa makamo hivi akasema ni HR Manager wa hiyo kampuni na kwa muda huo alikua headquarters ya hiyo kampuni kwa ukanda wa Africa zilizopo Nairobi Kenya, na mwingine alikua ni mkaka mzungu,akajitambulisha kuwa ni General manager wa hiyo kampuni kwa tawi la Africa ila kwa wakati huo alikua anaongea kutoka London zilipo ofisi zao kuu kwa duniani.

Kilichonishangaza ni aina ya hiyo interview how comes interview ifanyike kwa njia ya zoom wakati pale ofisini kwao kuna watu wangeweza kutufanyia interview?

Changamoto niliyoipata ni kwamba maswali yao nilikua siyasikii vizuri sababu spika zilikua haziko poa hivyo kunilazimu kuwa kila muda naomba muuliza swali aulize swali upya ili nipate idea ya anachokiuliza.

Pia interview yao kwa kukadiria imeenda dakika nyingi almost 15-20 minutes kitu ambacho kwa mimi niliyezoea interview za utumishi zinazolast 5-7 minutes nimeona ni mashikolo mageni.pia wanauliza maswali mengi sana, waliniuliza karibu maswali 15 hivi kwa kukadiria.

So naomba tuelimishane, interview hizi za njia ya zoom ziko sahihi kweli au ni kuchoshana tu?


Dunia imebadilika sana na enzi za kusafiri masafa marefu kwa ajili ya interview yamepitwa na wakati.
Pale ukiona tangazo na wakataka lazima ufike physically basi tambua umeapply shirika very outdated.
 
Back
Top Bottom