Rais Samia akutana na Wagombea Urais kutoka Vyama 16 baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025

Rais Samia akutana na Wagombea Urais kutoka Vyama 16 baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,809
Reaction score
15,034
wagombea.jpeg

WhatsApp Image 2026-04-01 at 15.56.46.jpeg

WhatsApp Image 2026-04-01 at 16.52.39.jpeg

WhatsApp Image 2026-04-01 at 16.52.31.jpeg

WhatsApp Image 2026-04-01 at 16.52.25.jpeg

WhatsApp Image 2026-04-01 at 16.52.54.jpeg

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAGOMBEA URAIS WA TANZANIA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 31 Machi, 2026, alikutana na wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akiitikia wito wao wa kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu hali ya kisiasa na masuala ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Viongozi hao kutoka vyama 16 vya siasa nchini walimtembelea Rais Dkt. Samia na kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuimarisha maridhiano ya kisiasa, demokrasia ya vyama, amani na mshikamano wa kitaifa baada ya Uchaguzi Mkuu, pamoja na namna ya kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na kudumisha tunu za umoja wa kitaifa.

Majadiliano hayo pia yaligusia umuhimu wa kuendeleza maadili ya uongozi, uwajibikaji na siasa zenye staha, kama msingi wa kujenga Taifa lenye utulivu wa kisiasa na maendeleo endelevu.

Katika kukuza demokrasia jumuishi, viongozi hao walisisitiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika masuala ya kitaifa na mchakato wa maendeleo, sambamba na kulinda utulivu wa kisiasa wakati wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kwa kutambua kuwa mazingira ya amani na umoja ni msingi wa ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Sambamba na hilo, walielezea umuhimu wa kuimarisha utamaduni wa uvumilivu wa kisiasa, kuheshimiana na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau wa kisiasa, kama njia ya kuendelea kudumisha utulivu wa nchi.

Hali kadhalika, walisisitiza haja ya kuendeleza mazungumzo ya mara kwa mara baina ya viongozi wa kisiasa ili kujenga uelewano wa pamoja na kushughulikia changamoto za kitaifa kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano, kwa kutanguliza maslahi ya wananchi na maendeleo ya Taifa.

Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza mawasiliano ya wazi na ya kujenga miongoni mwa viongozi wa kisiasa, kwa lengo la kuimarisha maridhiano na mshikamano wa kitaifa

Shaaban Kissu
K.n.y. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 31 Machi 2026, alifanya mazungumzo katika Ikulu ya Dar es Salaam na wagombea wa vyama vya siasa waliowania nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mazungumzo hayo yalifanyika kufuatia ombi lao la kukutana na Mkuu wa Nchi ili kujadili hali ya kisiasa na vipaumbele vya maendeleo ya taifa.

Viongozi hao, waliowakilisha vyama 16 vya siasa nchini, walimtembelea Rais Samia na kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuimarisha maridhiano ya kisiasa, demokrasia ya vyama vingi, amani, na mshikamano wa kitaifa katika kipindi cha baada ya uchaguzi. Pia walibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha ushiriki wa wananchi katika juhudi za maendeleo na kulinda tunu za taifa kama umoja na utulivu.

Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kuendeleza maridhiano ya kisiasa, kuimarisha demokrasia ya vyama vingi, kudumisha amani, na kuimarisha mshikamano wa kitaifa. Washiriki pia walisisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki wa wananchi katika maendeleo na kulinda misingi muhimu ya taifa ya umoja na uthabiti.

1775049271746.png

1775049289639.png
 
Maridhiano na wafuasi wa wagombea ambao hawakuona kama kuna shida ya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi? Watu sahihi wa kufanya nao maridhiano ni Chadema maana ndo hata uchaguzi hawakushiriki na wana wafuasi. Hawa wengine waliridhika.
 
View attachment 3565663
well done Dr.Samia Suluhu Hassan,
kazi na utu, tunasonga mbele na 4Rs
 
Maridhiano na wafuasi wa wagombea ambao hawakuona kama kuna shida ya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi? Watu sahihi wa kufanya nao maridhiano ni Chadema maana ndo hata uchaguzi hawakushiriki na wana wafuasi. Hawa wengine waliridhika.
Chadema hawautambui uchaguz wa 2025. Wanawezaje kukaa na kiongozi wasiyemtambua?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Anaendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa yeye ni chaguo la Mungu Aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe na aliyepewa kibali na Mungu kuongoza Taifa letu.

Anaendelea kuonyesha kuwa yupo kwa ajili ya ustawi wa Taifa na watanzania wote kwa ujumla wake. Kwa Hakika itatuchukua Miaka mingi sana kumpata kiongozi mzalendo na mwenye upendo wa Agape na Taifa hili

Embu soma hapa 👎
Screenshot_20260401-163327_1.jpg
Screenshot_20260401-163336_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi na viliyoshindwa huo uchaguzi vilivyoushiriki( uki ondoa chadema ambayo haikushiriki) vinatakiwa viungane vitengeneze chama kimoja cha upinzani..ccmb.

halafu hicho chama cha umoja wa vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi wa 25 na kushindwa...hicho chama kifanye maridhiano na ccm a juu ya uchaguzi walioushiriki.

chadema waachiwe huru mana hawakushiriki uchaguzi wala hawakuhisika na huo uchaguzi waachiliwe huru tu..na wala maridhiano hayawahusu kwa sababu hawakushiriki uchaguzi.
 
unaacha vyama 16 vilivyoshiriki uchaguzi na kushindwa uchaguzi halafu unaenda kuridhiana na chama kimoja tu ambacho hakikushiriki hata huo uchaguzi wenyewe.

ni sawa na simba na yanga zimecheza mpira dakika 90 zikaisha baada ya matokeo kutoka timu moja ikashinda nyingine ikashindwa.

sasa baada ya matokeo kutangazwa baada ya mechi kwisha ,maridhiano yanapaswa yafanyike baina ya simba na yanga timu zilizoshiriki mpira,sio mshindi anaenda kuridhiana na timu ambayo haikuwepo kabisa kwenye mashino.
 
1)mechi ilikuwa kati ya simba na yanga

2)baada ya dakika 90 za mchezo kwisha na matokeo kutoka mshindi akatangazwa.

3)mshindi wa mchezo anaenda kuridhiana na manchester united timu ambayo hata haikushiriki hiyo ligi./hayo mashindano
 
Back
Top Bottom