LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,481
- 36,618
Wimbo huu unaitwa Andrada, ulitoka mwaka 1996. Mimi nilikuwa darasa la tano wakati huo. Nikisikia wimbo huu nakumbuka vitu vingi sana, nawakumbuka rafiki zangu wa utotoni, na kikubwa zaidi namkumbuka huyu msichana anaitwa HALIMA HUSSEIN ( Jina la ukoo silitaji ), ambaye kwa mtazamo wangu nina amini ndio msichana mzuri kuliko wote duniani ambaye mimi nimewahi kumuona . Ni mixer mnyamwezi na msomali, ukikutana naye kwa mara ya lazima upige kelele. She was so so beautiful. Basi nikisikiaga wimbo huu huwa namkumbuka sana yeye. Kitu kingine namkumbuka sana aunty yangu, her name is Koleta, kwenye wimbo huu kuna segment inaimbwa " Koleta! Nyamaza!....." basi mayanki wa kitaani kwetu walikuwa wanamtania sana wimbo huu ukipigwa.. Hebu tukumbushane jama, mnakumbuka nini ?
Koffi Olomide- Andrada 1996 - YouTube
Koffi Olomide- Andrada 1996 - YouTube